"Ni ujasiri mkubwa kwa mtu mwenye jina kusimama na kusema, sababu wengi tunaona ni aibu kutambulika kama tunapigwa, na wanawake wengi hawasemi kwa sababu ukisema watu wanaanza kukuhukumu kwamba imekuwaje mpaka mume wako akupige" - Getrude Dyabene @humanrightstzKwa mujibu wa taarifa tuliyoitoa kuna zaidi ya kesi elfu 80 za matukio ya ukatili ambazo zimeripotiwa na matukio kama ya Shilole hayakuwepo kwa sababu hakusema na ni matukio yanayofanyika ndani" - Wakili Getrude Dyabene, Mkuu wa Dawati la Jinsia @humanrightstz
Jamii imemuweka mwanamke ana wajibu mkubwa wa kupigania ndoa au mahusiano yasimame, hivyo kuendelea kusimamia imani hiyo ndiyo imefanya wanaume waamini wana mamlaka ya kufanya chochote kwa mwanamke" - Getrude Dyabene, Mkuu wa Dawati la Jinsia @humanrightstz