Wananchi Wamkataa Aliyeongoza Kura za Maoni Rombo


Aliye kuwa diwani wa kata ya Chala kwa muda wa miaka mitano kwa mwaka 2010 wilayani Rombo mkoani kilimanjaro Clara joseph Gwandu Ameingia katika kashfa na mgogoro mkubwa na wananchi wa vijiji vya chala , mamsera kati na chini wakimtaka kurejesha rasilimali alizojimilikishia alivyotoka madarakani mara moja kabla majina ya wagombea kurudishwa katka kata na chama chamapinduzi wilaya ya Rombo

Wakiongea na vyombo vya habari wananchi hao wameleza kukerwa na diwani huyo wa kata kwa kuuza maeneo ya wananchi likiwemo eneo la Kidondoni kata ya Chala.

Ndugu waandishi wa habari sisi kama wananchi wa kata hii ya Chala tunaomba Dr Bashiru Ally kuangalia kura za maoni kwani tuna off kubwa sana mama huyu Clara Joseph kutumia rushwa kwa wajumbe kurudi madarakani kwa nguvu hata tumalizia rasilimali zetu.

Mpaka sasa amejimilikishia eneo pekee linalo toka matofali ya ujenzi katika machimbo eneo la vumbi la cement pamoja na msitu wa Kisereni wa kuvuna miti ya ujenzi ikiwemo na eneo la ziwa Chala ambapo mpaka sasa kuna mgogoro mkubwa na kijiji.

Endapo jina la diwani huyu litarejeshwa na CCM sisi tupo tayari kuchagua upinzani kwa sababu sio chaguo letu tutapigia kura upinzani Chadema au NCCR Mageuzi washinde kwani tumechoshwa na tabia zake za kujimilikishia mali za wananchi alisema bwana Prosper Limo.

Wananchi hao wameenda mbali wakasema kuwa kata hiyo iko mikononi mwa CCM kwa muda wa miaka mitano lakini sasa tutachagua upinzani endapo atutaletewa chaguo letu kwani Clara Alisa sababisha mwanzoni mwa mwaka 2015 kata kwenda Chadema Mara hii ameteuliwa tena kuwa mgombea wa CCM huku akiwa na mapungufu makubwa.

Clara katika uongozi wake alitumia madaraka yake kujinufaisha mwenyewe yeye pamoja na familia yake huku akishindwa kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo hospital Barabara pamoja na mambo mengineyo mengi.

Mpaka sasa wananchi wameandika barua ofisi ya CCM wilaya mara baada ya kuongoza katika kura za wajumbe zilizo fanyika hivi karibuni na Clara kuongoza katika kura hizo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad