Waziri "Umeme kwa matumizi ya kawaida ni Tsh. 100 kwa unit”



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, ametoa onyo kali kwa wazalishaji binafsi wa umeme, wanaowatoza wananchi gharama kubwa tofauti na bei elekezi.
Waziri amesema gharama ya umeme kwa wananchi wenye matumizi ya kawaida ni Tsh. 100 kwa unit moja.
Alisema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kahunda, Wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, alitoa agizo kwa Viongozi wa Serikali kuwachukulia hatua wazalishaji binafsi wa umeme, watakaobainika kukiuka agizo hilo.
Alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi, hasa wanaoishi visiwani hivyo Serikali haitavumilia tabia za baadhi ya wawekezaji binafsi kwani imewaamini kutenda haki katika kuwafikishia umeme wananchi ambao hawajafikiwa na Gridi ya Taifa.
Waziri aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa wawakilishi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa Jua ya Jumeme, baada ya wananchi wa kisiwa cha Maisome kuwatuhumu kuwauzia umeme kwa Tsh. 3,500 kwa unit moja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad