Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alaumu msimu wa baridi kuwa sababu ya ongezeko la corona Kenya


Msimu wa baridi unaoendelea huenda unachangia pakubwa ongezeko la watu wanaoambukizwa virusi vya corona nchini Kenya. 


Akizungumza baada ya kutangaza idadi mpya ya wagonjwa 544 waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini humo baada ya saa 24, waziri Afya Mutahi Kagwe amewataka Wakenya kutokongamana. 


Idadi hiyo amesema inajumlisha idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya kufikia 19,125. 


Wagonjwa hao wapya wanatokana na sampuli 5,259 zilizofanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24. 


Hiyo ina maana kwamba takriban watu 289,759 wamepimwa virusi vya corona nchini Kenya. 


Akizungumza katika makao makuu ya maafisa wa Afya mjini Nairobi, Kagwe amesema kwamba kijinsia walioambukizwa ni wanaume 340 na wanawake 204. 


lakini wagonjwa wengine 12 wameripotiwa kufariki kutokana maradhi hayo na hivyobasi kuongeza jumla ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia 311. 


Habari njema hatahivyo ni kwamba wagonjwa 113 wamepona na kuweka idadi waliopona kufikia 8,021

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad