Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Programu za Dharura wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa uzalishaji wa chanjo ya corona utachukua muda.
Dakta Mike Ryan amebainisha kuwa watafiti wako katika mchakato uliopiga hatua wa kuzalisha chanjo ya corona hata hivyo utengenezaji na utumiaji wa chanjo hiyo utachukua muda hadi mwanzoni mwa mwaka kesho.
Dakta Ryan ameashiria namna hivi sasa utengenezaji wa chanjo kadhaa za corona ulivyofikia katika marhala ya tatu ya majaribio na kwamba hakuna marhala iliyofeli kati ya hizo na kuongeza kuwa: Shirika la Afya Duniani linafanya kila linalowezekana ili kuwezesha upatikanaji wa chanjo zenye taathira dhidi ya virusi vya corona na kuzidisha uzalishaji wake.
Hadi sasa watu milioni 15 na 374,394 wameambukizwa virusi vya corona duniani na 630,211 wamefariki dunia kwa maradhi hayo ya Covid-19.
Aidha wagonjwa milioni 9 na 349,374 waliokuwa wamepatwa na maambukizi ya corona wamepona hadi sasa.