Wizara ya Afya Yaonya Kuhusu Kupuliza Kemikali Mitaani Kenya


Wizara ya Afya imeonya kuwa kupuliza madawa na kemikali kama inavyofanya katika baadhi ya maeneo haiondoi #COVID19, na ni hatari kiafya

Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara hiyo, Dkt. Patrick Amoth amesema haishauriwi kufanya hivyo, na kemikali hizo sio kwa ajili ya binadamu. Ameongeza kuwa zinaweza kusababisha matatizo ya upumuaji

Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO) kupuliza madawa sio njia sahihi ya kudhibiti #CoronaVirus na haipunguzi makali ya mtu kusambaza Virusi hivyo

WHO imeendelea kushauri watu kunawa mikono na maji pamoja na sabuni, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa, kuzingatia umbali salama na kubaki nyumbani inapowezekana ili kudhibiti maambukizi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad