Wizara ya Elimu imetolea ufafanuzi ongezeko la saa 2 za masomo kwa Wanafunzi baada ya Shule zote nchini kufunguliwa ili kufidia muda ambao umepotea kutokana na mlipuko wa CoronaVirus
Wizara hiyo imesema tathmini waliyofanya imebaini jambo hilo ni gumu kutekelezeka kwasababu kuna Shule zenye vibali vya kuendesha masomo kwa mfumo wa 'double shift'. Pia suala la usafiri kwa wanafunzi waishio mbali nalo limeonekana kuwa ni changamoto
Kutokana na hilo, Wizara imezitaka Shule kutumia ratiba za vipindi 8 kama ilivyokuwa awali na Shule zitakazoona umuhimu wa kuongeza muda wa masomo zitatumia muda uliopangwa kwenye ratiba zao