Nyota na nahodha wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania Xavi Hernandez amethibitisha kugundulikwa kuwa na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19
Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona, Xavi Hernandez (Pichani) akionyesha ufahari wa mataji (Treble) aliyotwaa akiwa klabu yake.
Xavi mwenye umri wa miaka 40 kwa sasa ni kocha wa klabu ya All Sadd ya nchini Qatar amesema kwa bahati nzuri anaendelea vizuri japo ataendelea kujitenga kwa muda hadi atakapokua amepona ugonjwa huo kama ambavyo utaratibu unaelekeza.
Kwa maana hiyo Xavi hatokuwepo kwenye benchi la ufundi wakati timu yake itakapoikabili Al Khor baada ya kocha huyo kuamua kujitenga kwa siku 7.
REKODI ZA KUVUTIA ZA XAVI ENZI ZA UCHEZAJI.
Kocha huyo ambaye anahusishwa na kurejea Hispania kuifundisha klabu yake ya zamani ya Barcelona, alikua na rekodi nzuri enzi zake akiwa mchezaji ambapo alicheza mechi zaidi ya 700, akifunga mabao 85.
Alikua ndiye mchezaji wa kwanza kucheza michezo 150 ya Ulaya na ile ya klabu bingwa ya Dunia kwa pamoja.
Xavi ambaye alikua ni kiungo mchezeshaji, alishinda mataji 8 ya La Liga na manne ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya