Yametimia....Putin Ashinda Kura ya Maoni; Atabakia Madarakani Hadi 2036
1
July 02, 2020
Rais Vladimir Putin ameshinda kura ya maoni ambayo itamuwezesha kubakia madarakani hadi 2036, wakati asilimia 78 ya kura zimekubali huku asilimia 90 ya kura zimekwishesabiwa, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya Urusi.
Putin mwenye umri wa miaka 67, amekuwa madarakani kama rais na pia waziri mkuu kwa miongo miwili na kwa hivi sasa ni rais aliyehumu nchini Urusi kwa kipindi kirefu zaidi ama kiongozi ya iliyokuwa jamhuri ya kisovieti tangu Joseph Stalin.
Russland Tver | Verfassungsreferendum | Coronavirus (picture-alliance/Sputnik/T. Makeyeva)
Mama mpiga kura akipiga kura yake katika kura ya maoni nchini Urusi
Kura ya maoni ilitaka kuidhinishwa kwa mabadiliko ya katiba ambayo yatamuwezesha Putin kugombea tena katika uchaguzi mara mbili zaidi na kuweza kubakia madarakani hadi akiwa na umri wa miaka 83. Muhula wake wa hivi sasa unamalizika miaka minne ijayo. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Urusi Ella Pamfilova amesema.
"Kwa mujibu wa data za awali, wapiga kura asilimia 65 walioandikishwa katika orodha ya wapiga kura walishiriki katika kura nchi nzima kuhusu mabadiliko ya katiba ya Urusi."
Putin amejijengea umaarufu kuwa ni mlinzi na kiongozi anayeweza kuleta uthabiti nchini humo, kinyume na hali ya kuyumba kwa uchumi na kisiasa katika kipindi baada ya iliyokuwa jamhuri ya kisovieti katika miaka ya 1990 ambayo imekuwa kabla ya kuingia kwake madarakani.
Hii inaonekana kama sababu muhimu katika kuidhinishwa kwa kura hiyo ya maoni. Watu wanapiga kura, kwa kutokuwa na kitu mbadala, kwa uthabiti," mtaalamu wa masuala ya Urusi Anna Arutunyan, mwandishi wa wasifu, "The Putin Mystique," Fumbo la Putin, aliliambia shirika la habari la Ujerumani DPA.
Putin ana uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa Warusi, akiwa na kiwango cha kukubalika cha asilimia 60 wiki iliyopita, kwa mujibu wa kituo kikubwa nchini humo cha kupima maoni ya wapiga kura cha Levada.
Putin, mrithi aliyeteuliwa na rais wa kwanza wa Urusi ya sasa, Boris Yeltisin, ameshinda chaguzi zote nne za urais, katika mwaka 2000, 2004, 2012 na 2018, kwa wingi mkubwa.
Russland I Irkutsk I Änderung der Verfassung (picture-alliance/dpa/A. Kushnirenko)
Bibi mtu mzima akitimiza haki yake ya katiba nchini Urusi ya kupiga kura
Ameshinda uchaguzi wake wa hivi karibuni kabisa kwa theluthi mbili ya kura, kiasi ya asilimia sawa kama ile ya kura ya maoni. Kura ya maoni ilikuwa na lengo la kutoa idhinisho la kidemokrasia kwa mabadiliko kadhaa, ambayo tayari yameidhinishwa na bunge la Urusi na kutiwa saini na rais Putin mapema mwaka huu.
Yamekuwa mabadiliko makubwa ya katiba ya Urusi tangu kuanza kutumika mwaka 1993 kufuatia kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti.
Tags
NA SISI TUTAFANYA HIVYO KWA MAGUFULI
ReplyDeleteWETU MZALENDO NA MCHAPAKAZI.