Yanga Yapeleka Mkataba wa Morrison FIFA



UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umepeleka mkataba wa kiungo wao, Bernard Morrison kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili waweze kuamua suala la utata wao.

Utata wa mkataba wa Morrison na Yanga umezidi kushika kasi ambapo kila upande unavutia kwao.

Morrison anasema mkataba wake na Yanga ulikuwa ni miezi sita tu na tayari umeisha, huku Yanga wakisema kuwa ana mkataba hadi 2022.

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa suala la Morrison uongozi umelichukulia kwa uzito jambo lililowafanya wapeleke mkataba wa mchezaji huyo CAF na FIFA.

“Tumepeleka mkataba wa Morrison CAF na FIFA, wao wana mamlaka kwenye masuala ya michezo, hatufanyi mambo kwa kubahatisha, hivyo hilo suala lake ninaweza.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, DAR
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad