Zidane Ataja Sababu Ya Kumtema Bale


KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amesema kukosekana kwa kiungo Gareth Bale katika sare dhidi ya Leganes, ilikuwa ni kwa sababu za kiufundi.

Bale aliachwa katika kikosi cha Madrid kilichotoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Leganes Jumapili iliyopita kwenye mchezo wa mwisho wa La Liga huku tayari mabingwa hao wakiwa wameshafanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Raia huyo wa Wales inaonekana ataondoka Real Madrid baada ya kucheza mechi mbili tu tangu kurejea upya kwa ligi huku akiwa hana maelewano mazuri na Zidane na akionyesha kitendo vya utovu wa nidhamu jukwaani kila anapotoswa kikosini.

James Rodriguez naye ametoswa katika mechi tano zilizopita huku zikitajwa sababu binafsi. Zidane kawazu ngumzia wote hao wawili.“Unajua nini kilitokea kwa mmoja (James). Mwingine ilikuwa ni kwa sababu za kiufundi,” alisema kocha huyo wa Real Madrid
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad