Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amelitaka jeshi la polisi na mwendesha Mashtaka wa Serikali kumuachia huru Nusrat na wenzake.
Nusrat ambaye ni kiongozi wa Bavicha wapi gerezani siku ya nane kwa tuhuma za kuimba wimbo wa taifa huku wakipandisha bendera ya taifa.
Zitto amesema ukandamizaji wa aina hiyo inaiweka nchi sehemu mbaya.
Kiongozi huyo alianfika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa “Acheni vijana hawa wafanye shughuli zao za kisiasa kikatiba,”
Jeshi la Polisi nchini @tanpol Pamoja na Mwendesha mashtaka wa Serikali DPP tafadhali sana mwacheni Huru Nusrat na mwezake. Ukandamizaji wa aina hii unaiweka Nchi yetu pabaya sana. Acheni Vijana hawa wafanye shughuli zao za kisiasa kikatiba. #FreeNusrat pic.twitter.com/ArrRQ0PwCM— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) July 18, 2020
Ivi kwa nn tunaishi kwa matukio ya kuichokoza serikali? Tufanye siasa za kistarabu tuache siasa za show hao wanaotushabikia hawana msaada wowote kwenye maisha yako, angalia sasa familia zenu ndo zinaangaika hao akina zito wanaishia kupiga kelele tweeter tu..
ReplyDelete