Zitto Kabwe "Naskia Aibu Kuwepo Bunge Lililopita"


The Economic History of the Mining Sector in Tanzania: An ...Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema anajisikia mwenye aibu kuwa mmoja kati ya wabunge waliotumikia bunge la 11 lilomaliza muda wake mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza kwenye mahujiano maalum na kituo cha redio cha Mashujaa mkoani Lindi, Zitto amesema Bunge hilo liliwekwa mfukoni na serikali na kuwadhurumu wananchi haki yao ya msingi.

“Bunge la 11 la Mheshimiwa Ndugai limekwisha hakuna hata muswada mmoja wa mbunge binafsi sio kwamba watu hawakupeleka walipeleka na ikazuiliwa isijadiliwe na hata kamati zilizoundwa hazaijawahi kutoa matokeo na hata kuiwajibisha serikali binafsi naskia aibu kuwa nimetumikia bunge la kumi na Moja”amesema Zitto.

Ikumbukwe kuwa bunge la Kumi na Moja lilioonhozwa na Spika Job Ndugai likifungwa rasmi  Juni 16,2020 na rais John Magufuli baada ya miaka mitano.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi najua kwa nini ujisikie hivyo.

    Sababu spika Ndugai ametendea haki nafasi ya kiiti na alidhibiti ipasavyo
    na wewe mpenda kiki hukupata kiki wala
    Umaarufu kama unavyo penda.

    Hili lilikuwa Bunge la Mfano.
    Spika Ndugai na mama Tulia wanastahili
    Pongezi Maradufu. Zitto una haha kwa
    lipi zaidi..?? Niseme Nisiseme!!??

    Kama umemuuzia Seif, Ruzuku atachukua
    alieleta na si wewe uliekosa Ubunge.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad