Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema Watanzania bado ni masikini katika nchi yenye kila aina ya utajiri.
Zitto amesema ukitazama mkoa wa Rukwa nusu ya watu ni masikini wa mahitaji ya msingi.
Zitto ambaye alikuwa Mbunge wa Kigoma Mjini aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter.
“Hawana uwezo wa kutumia hata shs 1500 kwa siku. Kutamba na uchumi wa kati ni kutukana watu,” aliandika Zitto.
Watanzania bado ni masikini sana katika Nchi yenye kila aina aina ya utajiri. Tazama mkoa wa Rukwa, karibu nusu ya Watu ni masikini wa mahitaji ya msingi, yaani hawana uwezo wa kutumia hata shs 1500 kwa siku. Kutamba na Uchumi wa Kati ni kutukana Watu. Hii ni #India2004 Vajpayee pic.twitter.com/nrwffzamCp— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) July 11, 2020