30 wakamatwa wakati wa maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu




Polisi nchini Israel imesema imewakamata waandamanaji 30 baada ya maelfu ya watu kuandamana mjini Jerusalem wakimtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujiuzulu, huku wakisema kwa sauti Waziri Mkuu mhalifu na kwamba ameshafutwa kazi. 


Waandamanaji hao walikusanyika nje ya nyumba ya Netanyahu jana usiku huku vyombo vya habari nchini humo vikikadiria waandamanaji kufikia 10,000. 


Kulingana na taarifa ya polisi iliyotolewa leo Jumapili, kulikuwa na vurugu katika maandamano hayo na baadhi ya maafisa walijeruhiwa. 


Waandamanaji watatu kati ya 30 waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo. 


 Netanyahu anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kufuatia madai kadhaa ya ufisadi dhidi yake na namna alivyoshughulikia janga la virusi vya corona, baada ya kuondoa masharti ya kutotoka nje mwezi Aprili hali iliyosababisha visa vya virusi hivyo kuongezeka nchini Israel. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad