Alichokiandika Lukaku Heshima kwa Vicent Kompany
0
August 18, 2020
Mshambuliaji wa Klabu ya Inter Milan, Romelu Lukaku ametoa heshima kwa nahodha wake wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji,Vicent Kompany ambaye ametangaza kustaafu kucheza soka.
Mkali wa mabao wa Inter Milan na Timu ya Taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku (Kushoto) akishangilia bao na Kocha wake Antonio Conte katika moja ya mchezo wa Serie A.
Kompany ametundika daruga akiwa na umri wa miaka 34 na moja kwa moja amekabidhiwa kazi ya kukinoa kikosi cha Klabu ya Anderletch ya huko kwao Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.
Lukaku ameandika kuwa ''umetufungulia njia wengi kati yetu ,nitakukumbuka sana kaka'' huo ndio ujumbe wa nyota huyo wa zamani wa Anderletch,Chelsea, Man United, Everton.
Kwa upande wa Klabu ya Manchester City ambayo aliichezea kwa miaka kumi na moja, lakini aliiogoza kama nahodha kwa miaka nane, wameandika hivi''hatotokea mwingine kama yeye,kila la kheri katika kustaafu wako''huo ni ujumbe kupitia mitandao ya kijamii ya City.
Enzi anaichezea Timu ya Taifa, Kompany alitumika katika michezo 89 na katika kizazi cha dhahabu alifika nayo hatua nzuri ingawa hakutwaa mataji na kikosi hiko.
Hivi sasa ametwaa nafasi ya Franky Vercauteren, huku mtendaji mkuu wa Klabu hiyo, Karel Van Eetvelt akisema kwamba kumteua Kompany ni mpango wao wa muda mrefu wenye leo wa kurejesha heshima ya timu yao.
Tags