Alichokisema Chirwa wa Azam kuhusu Yanga na Simba



Mshambuliaji bora wa Klabu ya Azam Fc kwa msimu uliopita, Obrey Chirwa ameufananisha ushindani uliopo kati ya Simba na Yanga ni kama uliopo huko nchini Hispania baina ya Real Madrid na Barcelona.


Chirwa ambaye alifunga mabao 12 katika ligi kuu amesema ushindani uliopo kwa vilabu vya Simba na Yanga ni mkubwa na umeleta chachu ya mpira wa Tanzania, ndio maana Vilabu hivyo vimekua vinatawala kwenye mbio za ubingwa wa hapa nchini kama ilivyo kwa Hispania kwa Real Madrid na Barcelona.

Nyota huyo Raia wa Zambia amesema Simba na Yanga zimejizolea mashabiki wengi kutokana na ushindani baina yao, ni sawa na Barcelona pia Real Madrid huko Hispania zilivyokusanya mashabiki wengi, kwa kuwa walijitengenezea kwa muda mrefu, nje ya uwanja na ndani wanafanya hivyo kila mwaka na hata ukizifuatilia ndizo timu zilizotwaa ubingwa wa La Liga mara nyingi kuliko timu zote zinazoshiriki .

Vile vile kwa hapa nchini Yanga imetwaa ubingwa wa ligi kuu mara 27 huku Simba ikiwa imetwaa mara 21 wakati Real Madrid ndio mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Hispania wakitwaa mara 36 huku Barcelona ikiwa imetwaa mara 26.

Anaamini kwamba Timu yake itafikia hatua hivyo kwa kuwakusanya mashabiki, kuwasajilia wachezaji wazuri,hivyo wataingia katika ushindani huo na kuwania ubingwa kwa asilimia kubwa.

Chirwa ambaye aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kutimkia Misri na kisha kurejea, ndiye mchezaji pekee aliyefunga Hat Trick kwenye michezo miwili msimu uliomalizika kiasi cha kupewa tuzo na Kandanda.com ikiwa ni kuheshimu uwezo wake aliouonyesha katika VPL.

TAKWIMU ZA MABINGWA LIGI KUU ZA HISPANIA NA YA TANZANIA BARA

Yanga ndio  Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu ya Tanzania Bara wakiwa wametwaa mara 27 huku Simba ikiwa ya Pili imetwaa mara 21.

Real Madrid ndio Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu ya Hispania wakiwa wametwaa mara 36 wakati Barcelona wametwaa mara 26.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad