Aliyeangushwa kwenye kura za maoni udiwani CCM Masasi ajiunga na CUF



   


   MGOMBEA udiwani kwenye mchakato wa kura za maoni chama cha Mapinduzi kata ya Mkuti Halmashauri ya mji Masasi, Roger Mbotela amekihama chama hicho na kujiunga na CUF na leo amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa chama cha wananchi (CUF)


  Mbotela ambaye katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM alipata kura 11 huku aliyeongoza kwenye mchakato huo alipata kura zaidi ya 100 dhidi yake, ambapo kwa matokeo hayo amedai kuwa yalimstajabisha na kwamba hakutarajia yeye kushindwa kwa kupata kura hizo chache.


    Akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani Maasasi mara baada ya kutangaza rasmi maamuzi hayo ya kujiunga na CUF Mbotela alisema uamuzi huo umekuja baada ya jina lake kushindwa kuchaguliwa kwa kura za kutosha na wajumbe ambapo katika mchakato huo alifanikiwa kupata kura 11 huku aliyemtangulia na kuwa mshindi kwenye mchakato huo wa kura za maoni alipata kura zaidii ya 100


   Alisema kutokana na wajumbe wa CCM walivyoshindwa kumpa kura za kutosha katika mchakato wa kura za maoni kama alivyokuwa ametarajia kumemsukuma kufanya maamuzi mapya nayo ni ya kukihama chama cha mapinduzi na kujiunga na wananchi cha wananchi CUF ambapo baada ya kuchukua kadi mpya ya CUF chama hicho kimekubali kumpa ridhaa ya kugombea udiwani katika kata hiyo ya Mkuti katika uchaguzi utakaofanyika oktoba 28 mwaka huu.


   Mbotela alisema awali kabla ya kutia ni ya kuingia kwenye kiny’ang’anyiro cha kugombea nafasi ya udiwani ndani ya CCM katika mchakato wa kura za maoni baadhi ya wajumbe wa CCM walimshawishi kuchukua fomu za kugombea kiti cha udiwani na kumpa ahadi kuwa wangemchagua kwa kura za kutosha lakini ameshangaa kwenye mchakto huo kupata kura 11   


    Alisema hakufurahishwa na matokeo hayo kwa vile hayakuwa matarajio yake kushindwa bali aliamini kuwa angeibuka kuwa wakwanza katika kuongoza kwenye uchaguzi huo wa kura za maoni lakini kilichotokea mara baada ya matokeo kutangazwa alishindwa hivyo hakuamni kuwa ameangushwa na wajumbe hao.


   “nimetumia haki yangu ya kikatiba kuhama CCM na kujiunga CUF ninachohitaji ni mabadiliko hivyo kwakuwa nimeangushwa kwenye kura za maoni katika chama cha mapinduzi basi nitayapata mabadiliko hayo ndani ya CUF ndio maana nimekuja huku kwani hakuna mtu anayezuiliwa kuhama chama chochote na kujiunga na chama kingine,”alisema Mbotela 


    Alisema amefanya kazi za chama akiwa CCM kwa zaidi ya miaka 15 na ni mwanachama halali wa chama hicho hivyo kitendo cha yeye kuangushwa kwenye kura za maoni katika mchakato huo wa kugombea udiwani ndani ya chama hicho una


   Kwa upande wake, mwenyekiti wa CUF wilaya ya Masasi Yusuph Matola alisema ni kweli wamempokea mwanachama huyo mpya na tayari wameshamkabidhi kadi ya chama hicho lakini pia wamempa ridhaa ya kugombea udiwani kata ya Mkuti.


    Alisema maamuzi ya CUF kuamua kumchagua kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya CUF katika nafasi ya udiwani kata ya Mkuti yametokana na kuona umaarufu wa mwanachama huyo kwa jamii katika kata hiyo ya Mkuti hivyo CUF inaamini itaweza kupata ushindi katika uchaguzi wa ujumla oktoba 28


   Naye katibu wa CCM wilaya ya Masasi,Shaibu Mtawa alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu mwnachama huyo kuhamia CUF alisema amesikia na kuona katika mitandao ya kijamii mwanachama huyo kuhama CCM na kuhamia CUF hivyo kwake sio jambo ngeni mwanachama kuhama CCM na kwenda chama kingine.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad