Amuua Ndugu yake wa Damu Kisa Makalio Makubwa ya Mwanamke

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna Warioba, ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake kuacha tabia hiyo mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji umesababisha kifo.

Kamanda Shanna amelazimika kusema hayo  hayo wakati akizungumza na kituo hiki akitolea ufafanuzi juu ya tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji  cha Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma Habibu ( 26).

Kwa mujibu wa Shanna Marehemu aliuwawa juzi majira ya saa mbili asubuhi wakati walipokuwa kijiweni na wenzake baada ya kutokea ugomvi kati yake na Ramadhani Habibu (23) ambaye ni ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa maumbile makubwa (makalio) kupita, mbele yao.

Alisema baada ya mwanamke huyo kupita mbele yao walianza mabishano ambapo marehemu alisema mwanamke huyo ana makalio makubwa na Ramadhani alisema ni makalio ya kawaida na makubwa.

Kamanda Shanna alieleza kuwa baada ya mabishano hayo ndipo ulipozuka ugomvi hadi kufikia hatua ya Ramadhani kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kuliana na alifariki dunia akiwa njiani anapelekwa hosptali ya kisarawe.

Alisema jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kuwa atafikishwa mahakamani mara moja  na kuwa amekubali kuwa amefanya mauaji hayo.

Kufuatia,tukio hilo kamanda Shanna aliendelea kutoa onyo kwa wananchi na  vijana wanaoshinda vijiweni kuacha tabia ya udhalilishaji hasa kwa wanawake na kuwa ni kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwa kama kuna mtu aliyefanyiwa vitendo vya namna hiyo atoe taarifa polisi na atafikishwa mahakamani.

"Wito kwa wale wanaokiuka haki za binadamu kwa kumdhalilisha mtu waache mara moja, mfano kisheria hata kumkonyeza mtu ni kosa la jinai hivyo unapaswa kufika polisi, na tutamfuatilia kisha kumpeleka mahakamani" Kamanda Shana amefafanua

Pia kamanda Shanna ametoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao ili kuepusha vishawishi na matamanio kwa wanaume
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad