Baada Ya Ukimya Lijulikali Atema Cheche " Urais wa Nchi yetu sio huruma"


Peter Lijualikali Aendelea Kuikalia Kooni Chadema Afunguka Mengine ...Aliyekuwa mbunge wa Kilombero (CHADEMA) Peter Lijualikali amefunguka kuwa cheo cha urais wa Tanzania sio pole kwa mgonjwa wala sio huruma bali ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa mzalendo cha nchi yako.

Lijualikali ametuma ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa twitter na huku akichapicha na picha ya kuonyesha kuunga mkono rais Magufuli kwenye kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  mapema mwezi Oktoba.

“Urais wa Nchi ya Tanzania sio Pole kwa Mgonjwa. Urais wa Nchi yetu sio huruma. Urais wa Nchi yetu ni matokeo ya uchapakazi, uwajibikaji, uzalendo na uadilifu kwa Taifa letu. Ni Magufuli Tena 2020-2025!, Viva CCM, Viva Magufuli, Hapa Kazi Tu” amendika Lijualikali.

Lijualikali alitangaza kukiama chama chake cha CHADEMA na kujiunga na CCM siku chache kabla ya kumalizika kwa vikao vya bunge la 11 jijini Dodoma na hakufanikiwa kuchaguliwa kwenye mchakato wa awali wa chama hicho kuchagua mgombea ubunge kwenye jimbo la Kilombero.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad