Mfahamu Baharia wa Meli, Idara za Meli na Nafasi za Mabaharia Katika Meli
0
August 19, 2020
Baharia (Seafare) ni mfanyakazi yeyote katika meli.Katika meli kuna mabaharia ambao ni maofisa(Officers) na ambao si maofisa(Crew).
Meli ina idara kuu 3 kulingana na mgawanyo wa majukumu na vitengo.
1.DECK DEPARTMENT (Kuongoza meli)
2.ENGINE DEPARTMENT (Wahandisi wa meli)
3.CATERING DEPARTMENT ( Huduma za vyakula)
NAFASI ZA AJIRA 98 MPYA ZILIZOTANGAZWA BONYEZA HAPA
1. DECK DEPARTMENT
Hii ni idara inayohusika na uongozaji wa meli.Hawa ni mabaharia kuanzia maofisa mpaka wafanyakazi wa kawaida na majukumu yao.
Master/Captain (Nahodha)
Huyu ni kiongozi mkuu katika meli na yeye ndio msemaji wa mwisho. Ni mwakilishi wa mmiliki wa meli sehemu anapokuwa na meli. Ni mwakilishi wa nchi ambayo meli inapeperusha bendera iliyosajiliwa.
Majukumu yake ni kusimamia shughuli za kila siku za meli,hali ya amani katika chombo na kusaini documents kama bill of lading ya mzigo.Kusimamia sheria na taratibu kwa watu wote melini na kuwepo sehemu ya kuongozea na kutoa maagizo wakati wa meli kuingia na kutoka eneo la bandari.
Chief Officer
Huyu ni ofisa anayefuata baada ya nahodha wa meli, ana vyeti sawa na nahodha pia akifanya kwa kipindi kirefu anakidhi kupewa unahodha wa meli. Chief officer anaripoti kwa nahodha.
Majukumu yake ni kusimamia na kuandaa cargo plan, yeye ni incharge wa mabaharia wote walio chini yake. Kusimamia majukumu ya mawasiliano ya radio katika meli,matengenezo ya meli.
Second Officer
Huyu ni afisa anayefata baada ya Chief officer na anaripoti kwa Chief officer.
Majukumu yake ni kusimamia uchoraji wa route ya safari,ramani za safari na vifaa vya kuongozea meli. Huyu pia ni incharge wa vifaa vya mawasiliano ya radio na anafanya kazi kama afisa afya.
Third Officer
Huyu ni afisa anayefuata baada ya Second Officer.
Majukumu yake ni kusimamia vifaa vya uokoaji na vifaa vya kuzimia moto,kuandaa ripoti ya drill zifanyikazo melini, kumsaidia Chief Officer wakati wa kupakia na kupakua mizigo. Kusimamia sehemu za ufungaji kamba katika meli.
Deck Cadet
Huyu afisa mwanafunzi katika idara ya uongozaji meli. Anajifunza kazi na anakuwa chini ya uangalizi wa chief officer. Na anafanya kazi mbalimbali za usafi,kupaka rangi na kamba.
Mabaharia wasio maofisa
Bosun
Huyu ni kiongozi mkuu wa mabaharia wa kawaida melini.
Majukumu yake ni kusimamia usafi,upakaji rangi,kazi za kufunga kamba,kusimamia stoo na kumsaidia chief officer wakati wa kuweka nanga. Pia anaripoti kesi za utovu wa nidhamu za mabaharia kwa Chief Officer.
Able-Bodied Seaman (AB)
Huyu ni baharia wa kawaida ambaye majukumu yake ni usafi,kupaka rangi, kazi za kamba na kushika usukani wa meli pia kumsaidia afisa wa zamu wakati meli inapotembea.AB mzoefu anaweza akapanda mpaka kuwa Bosun.
Ordinary Seaman
Huyu majukumu yake ni usafi, kugonga kutu, kupaka rangi na kazi za kamba.
Huyu haruhusiwi kushika usukani meli inapotembea wala kukaa zamu sehemu ya kuongozea meli.
2. ENGINE DEPARTMENT
Hii ni idara inayohusisha wahandisi wa meli ambao ni maofisa na baharia wa kawaida wenye ujuzi wa ufundi wa meli.
Chief Engineer
Huyu ni kiongozi mkuu katika idara ya injini.
Majukumu yake ni kutoa oda na kusimamia kazi zote engine room. Kuandaa ripoti za kiufundi kuhusu meli kwenda kwa mmiliki.Kufanya mahesabu ya mafuta, kusimamia sheria eneo la chumba cha injini na kuripoti hali yoyote ya hatari kwa nahodha.
Second Engineer
Huyu ni injinia baada ya chief injinia.
Majukumu yake ni kumsaidia Chief injinia, incharge wa mashine zote kama injini, jenereta, pampu na steering gear.Kuandaa orodha ya marekebisho na kupanga ratiba ya marekebisho.
Third Engineer
Majukumu yake ni kusimamia na marekebisho ya jenereta, boiler, kuangalia mifumo ya boiler na maji.
Fourth Engineer
Majukumu yake ni kusimamia ujazaji mafuta na kumsaidia chief ofisa katika mahesabu ya mafuta. Kusimamia shughuli za mtambo wa maji taka, uchomaji taka, maji safi na mtambo wa kuchuja maji na oil.
Engine Cadet
Huyu ni afisa mwanafunzi katika idara ya injini na anakuwa chini ya usimamizi wa Second Officer. Majukumu yake ni usafi chumba cha injini na kusimamia uendeshaji wa injini meli inapotembea.
Mabaharia wa kawaida katika idara hii
Fitter
Huyu ana ujuzi wa kuchomelea, kukata vyuma,kutoboa na kuchomela kwa gesi. Huyu anafanya kazi chini ya Second officer.
Oiler
Huyu anafanya kazi za marekebisho katika injini, aawasaidia mainjinia wakati wa kufungua injini,kufanya usafi na kupaka rangi.
Wiper
Kazi yake kubwa ni kufanya usafi eneo la injini.Anafanya kazi ya kuwasaidia mainjinia wakati wa marekebisho ya injini.Akipata uzoefu wa kutosha hupewa nafasi ya oiler.
3.CATERING DEPARTMENT
Hii idara inashughulika na chakula na usafi wa maeneo ya kulia chakula (Mess).
Chief Steward
Majukumu yake ni kupanga ratiba za usafi wa mess, ratiba ya chakula na usimamizi. Pia anajukumu la kuangalia overtime za watu na kipindi cha nyuma yeye alikuwa akitumika kugawa posho na mishahara.
Chief Cooker
Huyu ni mpishi mkuu katika meli, majukumu yake ni kupika vyakula na kuandaa ratiba ya chakula. Kupika vyakula kulingana na mapishi ya mataifa mbalimbali ya wafanyakazi katika meli na kumsadia nahodha kutoa orodha ya mahitaji katika idara anayosimamia. Anapaswa ajue lugha na mapishi ya vyakula mbalimbali.
Stewards
Huyu ni msaidizi wa mpishi mkuu na anasaidia shughuli za kupika, kufanya usafi na kuandaa chakula. Pia anafanya kazi ya kufanya usafi vyumba vya maofisa, kusimamia ugawaji chakula.
Galley Boy
Huyu huwa baadhi ya meli kazi yake kubwa ni kuosha vyombo jikoni na kufanya usafi. Pia hushiriki kukata mboga, nyanya na vitunguu. Huwa ni mtu asiyepewa heshima sana na kudharaurika katika meli.
NAFASI ZA AJIRA 98 MPYA ZILIZOTANGAZWA BONYEZA HAPA
SARE ZA MABAHARIA
Mabaharia ambao ni maofisa huvaa shati yenye rangi nyeupe,bluu au kaki ikiwa na beji pembeni ya bega la kulia na kushoto. Wale wa upande wa uongozaji kuanzia Nahodha yeye huwa na alama ya nanga au usukani na mistari 4. Anayefuata mistari 3,2,1 na Cadet yeye mstari wake huwa ni mmoja uliolala.
Pia upande wa engine Chief engineer huvaa beji yenye alama ya propela ya meli na mistari 4, Second engineer 3, Third engineer 2, Fourth engineer 1 na Cadet engineer ni mstari 1 uliolala.
Kwa mabaharia wasio maofisa wao hawavai beji nguo zao begani huwa hazina kitu. Tisheti za mabaharia zote ni sawa kwa ngazi ya ofisa na wa kawaida.
Tags