WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mwandisi Isack Kamwele ametegua uteuzi wa maneja wawili wa mikoa ya Lindi na Pwani kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ya kusimamia miundo mbinu ya barabara kwenye mikoa yao .
Kamwele alichukua uamuzi huo juzi akiwa njiani kutoka Inyonga kwenda Mkoani Lindi wakati akikagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha rami yenye urefu wa kilometa 1.6 inayotoka Kibaoni kwenda makao makuu ya Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi
Aliwataja mameneja aliowasimamisha kazi kuwa ni Mwandisi Isack Mwanawima ambae ni Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa Lindi na Yudas Msangi ambae ni Kaimu Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa Pwani .
Maagizo hayo ya kuwasimamisha kazi aliyatowa ikiwa ni siku moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kuonekana kutoridhishwa na hali ya barabara za mikoa hiyo.
Rais Magufuli alitumia barabara hizo wakati akitokea mkoani Mtwara kwenye mazishi ya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa.
Kamwele alisema Rais alipita kwenye barabara ya Miginyo hadi Lindi amekuta barabara ya lami lmeharibika sana imekuwa kama barabara ya vumbi wakati fedha za matengenezo zipo.
“Pia hata barabara hiyo inayopitia kwenye Mkoa wa Pwani nayo imeharibika hivyo kwa mamlaka niliyopewa na Rais, mameja wa mikoa hiyo yote miwili anawasimamisha kazi.
Katika hilo alisema ni jambo la aibu kuona barabara zinaharibika na Rais aliyepita kuziona wakati na mameja hao wapo.
Alisema jambo hilo ni la aibu hata kwake na halijamfurahisha na ndio maana ameamua kuchukua uamuzi huo.
Mwandisi Kamwele alisema Tanroads walikuwa na sifa nzuri lakini wameanza kuharibiwa na watumishi wachache.
“Kwa hiyo watambue kuwa kipindi hiki sio cha kufanya mchezo kila anae bainika kushindwa kutekeleza wajukumu yake atambue kuwa atawajibishwa,” .
Aliwaagiza mameja wa Tanroads kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu barabaara zote ambazo ziliharibiwa na mvua za msimu huu matengenezo yake yawe yamekamilika.
“Wizara ya ujenzi imeishatoa kiasi cha shilingi bilioni 35 kwa ajili ya matengenezo ya barabara hizo kwa meneja atakaeshindwa kukamilisha matengenezo hayo ajue kuwa kazi yake ya umeneja ndio mwisho wake siku hiyo ya agosti 30,” alisema.