Binti wa Miaka 17 Mahakamani: Sikubakwa na Nilitaka Mwenyewe



MTOTO wa miaka 17, ameiambia Mahakama ya Mkoa ‘B’ Chake Chake kuwa, mshitakiwa Bakar Mbwana Juma wa Kengeja hakumbaka, bali aliridhia mwenyewe kufanya nae tendo la ndoa, kama njia ya kumridhisha mpenzi wake huyo.


 


Akitoa ushahidi wake Mahakamani hapo, alidai kuwa baada ya kufika nyumbani kwa mshtakiwa huyo kwa lengo la kufanya nae mapenzi, kwanza alikataa.


 


Alidai kuwa, baada ya kukataa na kufanya nae mapenzi, alifanya kama anarudi nyumbani kwao, kisha aliamua kurudi nyumbani mwa mshitakiwa huyo na kumvulia nguo.


 


Alidai kuwa, mara baada ya kumvulia nguo na kumalizia kufanya nae tendo, wakiwa chini sakafuni, aliamua kurudi nyumbani kwao majira ya saa 2:00 usiku akiamini kuwa ameshamridhisha mpenzi wake (mshtakiwa).


 


“Nilipofika nyumbani Mama kwa vile sikumuaga, aliniuliza natoka wapi, lakini sikumwambia na alipokuja Kaka yangu baada ya kunitishia kunipiga pia nilikaa kimya, sasa safari ikawa ni Kituo cha Polisi, ingawa njiani niliwambia ukweli,’’ alidai.


 


Mtoto huyo aliendelea kuiambia Mahakama hiyo kuwa, wakati wakiwa njia anapelekwa kituo cha Polisi Kengeja, aliwaeleza alipokuwa na kisha alihojiwa Polisi, na siku ya pili alipelekwa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani kwa uchunguuzi zaidi.


 


Alidai kuwa, amekuwa hana kawaida ya kumuaga mzazi wake yeyote anapokwenda safari ya karibu, ingawa kwa safari za mbali, anao utamaduni wa kuomba ruhusa.


 


Awali mtoto huyo ambae ni shahidi namba mbili kwenye shauri hilo alida kuwa, amekuwa na mazoea ya muda mrefu na mshitakiwa, ingawa tendo la ndoa amefanya siku moja tu ambayo alipata maumivi makali.


 


Mara baada ya wakili wa serikali Juma Ali Juma kumaliza kumuongoza shahidi huyo kutoa ushahidi wake, Hakimu wa mahakama ya mkoa ‘B’ Chake Chake, Luciano Makoye Nyengo aliupa nafasi upande wa mashtaka, kumuuliza maswali shahidi huyo.


 


Hakimu huyo, kisha aliliahirisha shauri hilo na kumtaka mshitakiwa huyo kurudi tena mahakamani hapo Agosti 11 mwaka huu , na kuutaka upande wa mashtaka kuwasilisha mashahidi waliobakia siku hiyo.


 


Awali ilidaiwa kuwa, mshitakiwa Bakar Mbwana Juma miaka 32, alidaiwa kumtorosha mtoto huyo mwenye miaka 17 kutoka nyumbani kwao na kwenda nae kwenye nyumba anayoishi, huko huko Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba.


 


Tukio hilo lililotokea Juni 2, mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku, ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu 113 (a) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018.


 


Kosa la pili kwa mtoto huyo, mwenye miaka 17 siku hiyo hiyo, baada ya kumtorosha alimbaka, ambapo hilo ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya adhabu nambari 6 ya mwaka 2018.


 

OPEN IN BROWSER

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad