Chama la Yanga CAF Hili Hapa



UPO uwezekano mkubwa wa Yanga kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuiondoa nchi ya Libya katika ushiriki wa michuano ya kimataifa.


 


Yanga na Azam wamekuwa na tegemeo kubwa la kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao kutokana na Nchi ya Libya kufuta ligi zake kufuatia kuwepo kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo imesababisha kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).


 


Ipo hivi Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi 12 ambazo zina nafasi ya kupeleka timu nne katika michuano ya Caf ambapo Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 14 kabla ya kuzidiwa na Libya ambayo imepanda kwa nafasi sita na kuwa timu ya 12 ikiwa na pointi 16.5 huku Tanzania ikishuka hadi nafasi ya 13 ikifuatiwa na Ivory Coast wenyewe pointi 13.5.




Yanga hivi sasa inasubiria taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo nalo linasubiria kutoka Caf kabla ya kuzitaarifu timu hizo juu ya ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa.


 


Wakati Yanga wakisubiria taarifa rasmi, tayari inaendelea kukiimarisha kikosi chake ambacho kinajiandaa na michuano hiyo mikubwa ya kimataifa ili kuhakikisha wanafanya vema.


 


Kikosi cha Yanga ambacho huenda watakitumia katika michuano hiyo ni Farouk Shikalo ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa katika kikosi cha kwanza, beki wa kulia Shomari Kibwana, beki wa kushoto Yassin Mustapha na mabeki wawili wa kati ni Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto.


 


Kiungo mkabaji namba sita ni Mukoko Tonombe, winga wa kulia Tuisila Kisinda, kiungo mchezeshaji namba nane Feisal Salim ‘Fei Toto’, namba tisa Yacoub Sogne, namba kumi Heritier Makambo na winga wa kushoto ni Farid Mussa.Wakati wachezaji wa akiba wakiwa ni Metacha Mnata, Paul Godfrey ‘Boxer’, Zawadi Mauya, Muadjiri Hakizimana, Haruna Niyonzima, Waziri Junior na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.




Kwa upande wao Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wao, Fredrick Mwakalebela amesema: “Kama itatokea Tanzania ikapata nafasi ya uwakilishi wa timu nne Caf na Yanga kupata nafasi hiyo basi tutakuwa tayari kushiriki kwani tumefanya usajili mzuri wa wachezaji wa ndani na nje, hivyo tuna kikosi imara.


 


“Pia kwenye ligi tuliweza kupambana hadi tukamaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi, hivyo itakuwa ni heri kwetu na iwapo itatokea tukaipata hiyo nafasi tutafanya vyema katika mashindano hayo.“Timu tayari imeshaanza mazoezi na inakwenda vizuri na wakati wowote tunatarajia kumtangaza kocha mkuu.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad