Chanzo Uwoya Kutembelea Magongo

 


SIKU chache baada ya kusambaa picha zinazomuonesha mrembo wa filamu nchini Irene Uwoya, akitembea kwa kutumia magongo, imebainika kuwa chanzo cha msanii huyo kuteguka mguu, ni mihangaiko yake katika maisha.


 


Picha hizo ambazo ziliibua hofu kwa mashabiki wake ambao wengi walitaka kufahamu chanzo na hali yake kiafya, RISASI limepata uhondo wote.


 


Akizungumza na gazeti hili msanii mwenzake ambaye pia ni rafiki yake wa karibu; Blandina Chagula ‘Johari’, alisema chanzo cha mwanamama huyo kutembelea magongo, ni kuwa aliumia.


 


“Uwoya aliumia mguu wakati wa mihangaiko yake ya hapa na pale, ndiyo maana unaona akawa amefungwa mguu na anatembelea magongo, lakini Mungu mwema kwa sasa anaendelea vizuri,” alisema Johari.

Mrembo huyo ana muda hajaonekana mitandaoni kwa madai ya kuwa, akaunti yake ya Instagram imepata matatizo, hivyo anaishughulikia.


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad