Donald Trump: Siitaki TikTok ya Wachina Marekani, mamlaka ya kuifungia ninayo



Rais wa Marekani Donald Trump ameeleza kuwa siku ya jumamosi hii ataufunga rasmi mtandao wa TikTok na kudai kuwa hautatumika tena nchini Marekani kutokana na mtandao huo ni wa Kichina


Trump ameongeza kuwa “Nitaipiga marufuku TikTok kutumika hapa Marekani na Mamlaka hayo ninayo na sitaki Kampuni za Marekani zinunue mtandao huo” akiongeza kuwa


Inaelezwa Microsoft imeonesha nia ya kuinunua TikTok”


Hayo yanakuja baada ya kuelezwa kuwa mtandao wa kijamii ambao ni TikTok original yake ikiwa ni China na China na Marekani kama inavyofahamika wako kwenye msuguano mkubwa wa kiuchumi pia inatajwa kuwa mtando huo ni tishio kubwa sana kwa usalama na Wamarekani ikielezwa  kuwa Serikali ya China inautumia mtandao huo kudukua na kufuatilia mawasiliano ya Raia wa Marekani na maeneo mengine wanaotumia mtandao huo na kusema huenda ukatumika kuingilia uchaguzi.


Haikubainika mara moja ni mamlaka gani aliyonayo Trump ya kupiga marufuku TikTok, vile marufuku hiyo itakavyotekelezwa na changamoto za kisheria anazoweza kukumbana nazo.


Inasemekana kwamba kampuni ya Microsoft imekuwa ikifanya mazungumzo ya kununua programu hiyo kutoka kwa kampuni ya ByteDance, lakini Bwana Trump ameonekana kutilia mashaka kuwa makubaliano kama hayo yanaweza kufanyika.


Ikiwa makubaliano hayo yataafikiwa, taarifa zinasema kwamba itajumuisha kampuni ya ByteDance kumaliza shughuli zake kupitia programu ya TikTok Marekani.


Msemaji wa programu ya TikTok amekataa kuzungumza lolote dhidi ya hatua ya Trump lakini amearifu vyombo vya habari kwamba kampuni hiyo ina matumaini makubwa ya mafanikio ya muda mrefu Marekani.


Hatua ya kupiga marufuku programu ya TikTok inawadia wakati ambapo kuna wasiwasi kati ya utawala wa Trump na serikali ya China kuhusu masuala kadhaa ikiwemo mzozo wa kibiashara na vile China ilivyoshughulikia mlipuko wa janga la virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad