Drone zinaweza kutumika kuihujumu nchi- Polisi



 Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania SACP David Misime, amesema kuwa ndege zisizokuwa na Rubani maarufu kama drone zisiposajiliwa zinaweza kutumiwa kwa nia ovu ili kuihujumu nchi huku pia ikielezwa kuwa zinaweza kutumika kama silaha na kuleta maafa kwa Taifa.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo ambapo katika kutekeleza hilo Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania na Jeshi la Polisi kwa pamoja wameamua kushirikiana na kuunda kikosi kimoja, ambacho kitaweza kusimamia utekelezaji wa kanuni ambayo inawataka wamiliki wote wa Drones kuzisajili.


“Drone zinaweza kutumika kuihujumu nchi kwa kuchukua taarifa kwa nia ovu, hivyo ukikamatwa unaiendesha bila kibali ni kosa la jinai kama yalivyo makosa mengine” Misime


“Ni kweli tupo katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia, lakini teknolojia zingine lazima tuhakikishe tunadhibiti madhara yanayoweza kujitokeza mbeleni na hii ni kwa faida ya Watanzania wote” Misime


Mbali na hayo imeelezwa kuwa ikibainika mtu anatumia drone bila kusajili, adhabu yake ni faini ya Shilingi Milioni Moja au kifungo cha miezi sita jela.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad