Facebook, Twitter zaondoa ujumbe wa Trump kuhusu virusi vya korona
0
August 06, 2020
Mitandao ya Facebook na Twitter imeondowa ujumbe wa Rais Donald Trump ambao imesema unavunja kanuni zinazokataza kusambaza habari za kupotosha juu ya virusi vya korona.
Ujumbe huo ulikuwa na kipande cha vidio kutokana na mahojiano yake na Fox&Friends, ambapo Trump anadai kuwa watoto wadogo wana kinga dhidi ya COVID-19.
Msemaji wa Facebook amesema kuwa ujumbe huo ni wa uongo. Ujumbe wa Twitter wenye vidio hiyo hiyo ambao awali ulitumwa na timu ya kampeni ya Trump nao pia ulifichwa na Twitter kwa sababu hizo hizo.
Msemaji wa Twitter amesema timu hiyo ya kampeni inapaswa kwanza kuuondowa ujumbe huo kabla hawajaruhusiwa tena kuutumia mtandao huo.
Kituo cha Udhibiti wa Maradhi nchini Marekani, CDC, kimesema hata kama watu wazima ndio waathirika wakubwa wa maambukizo ya virusi vya korobna, haimaanishi kwamba watoto wako salama, kwani kuna visa vingi vya wao kupoteza maisha pia.
Tags