Fahamu Dalili za mtu kujifungua Mtoto wa Kiume


Kumekuwa na shauku ya wazazi kujua ni jinsia gani ya mtoto ambaye anatarajiwa kuzaliwa, sasa kupitia kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio mtangazaji Mwanne Othman ametoa dondoo kuhusiana na ishara za kujifungua mtoto wa kiume endapo mwanamke anapokuwa mjamzito.

Sasa kupitia kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio mtangazaji Mwanne Othman ametoa ishara za kiasili za kutambua kama mtoto aliyetumboni anaweza akawa wa kiume wakati wa kuzaliwa.

"Ishara za kujifungua mtoto wa kiume kwa mwanamke mjamzito kwanza magonjwa ya asubuhi mfano kusikia kichefuchefu asubuhi, mapigo ya moyo kuongezeka, kutokwa na chunusi, hamu ya chakula vichachu na vyenye chumvi na mkao wa tumbo kama upo chini" ameeleza Mwanne Othman

Aidha ameendelea kusema "Kingine ni mabadiliko ya tabia, mama wenye hasira watapata watoto wa kiume, rangi ya haja ndogo kubadilika, matiti kuwa makubwa la kulia ni kubwa kuliko la kushoto, miguu kuwa ya baridi, kukua kwa nywele, namna ya kulala na kuongezeka uzito".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad