Mara nyingi tumekuwa tuki-chaji simu mpya kwa muda wa masaa sita huku wengine wakiacha simu kukesha kwenye chaji.
Kitaalumu zaidi, yawzekana wanaotuambia huenda hawafahamu vizuri masuala ya Teknologia ya vitu hivyo, hali inayopelekea kuharibu betri ya simu pasipo kutambua kwamba kama unaiharibu betri yako ambayo ingeweza kudumu muda mrefu kwa matumizi ya simu yako.
Zifuatazo ni njia zakufanya ukisha nunua simu yenye betri mpya ama betri mpya:
a) Hakikisha unaiwasha kwanza simu hiyo na kujua ina aslimia ngapi. Kama utaiwasha na kuikuta ina chaji asilimia 49% na kushuka chini, unashauriwa uizime na uichaji simu hiyo kwa muda wa masaa matatu. Kwa kuchaji muda huo, itasaidia betri kujaa vizuri zaidi.
b)Endapo umewasha na ukakuta betri asilimia 50% na kuendelea juu, unashauriwa kuitumia simu hiyo mpaka chaji ifike asilimia 10% na kisha uichaji kwa masaa matatu ili iweze kujaa vizuri zaidi.
c)Kila ifikapo asilimia 10% ya chaji ni muhimu kukumbuka kuichaji simu yako, unashauriwa kuichaji simu yako hiyo ikiwa imezimwa kwa masaa mawili. Kwa kuzingatia hayo Betri ya simu yako itadumu kwa muda mrefu.
Epuka kuchaji simu yako mara kwa mara kwa kuhofia chaji kwani kufanya hivyo humaliza nguvu ya betri yako kwenye simu. Pia usiweke simu yako karibu na vitu vinavyoweza kuua nguvu ya betri.