Farid na Yanga ni Suala la Muda Tu


INAELEZWA kuwa Yanga iko kwenye mazungumzo mazuri na mchezaji wa zamani wa Azam na CD Tenerife ya Hispania, Farid Mussa ili kukamilisha dili la usajili unaotarajiwa kutangazwa muda wowote baada ya mchezaji huyo kumwaga wino.

Chanzo cha kuaminika ndani ya Yanga kilisema kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea vizuri na kilichobaki kwa sasa ni suala la muda tu ili kuona kama wataweza kufi kia makubaliano au la.

“Ni kweli upo mpango wa kumsajili Farid Mussa kama sehemu ya kuimarisha kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao na tayari uongozi unaendelea na mazungumzo na mchezaji husika.

“Hivyo kama pande zote zitaafi kiana basi ishu ya Farid kuvaa uzi wa Yanga kwa msimu ujao itabaki kuwa suala la muda tu,” kilisema chanzo hicho.

Spoti Xtra, lilimtafuta Farid ambaye alikiri kuhitajika na baadhi ya klabu lakini kuhusu wapi atasaini, alisema kila kitu kitakuwa wazi hivi karibuni.

“Ni kweli nimekuwa nikihusishwa kujiunga na baadhi ya klabu hapa nchini kutokana na ukweli kwamba mimi ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kuachana na CD Tenerife.

“Ni mapema sana kusema ni wapi nitaelekea lakini mambo yakiwa sawa basi kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Farid

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad