Fedha zilizochangishwa na JPM zawasilishwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Magufuli leo Agosti 24, 2020, amewasilisha fedha za michango iliyotolewa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino Mkoani Dodoma.


Katibu wa Rais Ngusa Samike akimkabidhi Sheikh Mkuu wa Wilaya Suleiman Abdallah Matitu, fedha zilizochangishwa na Rais Magufuli.

Fedha hizo zimewasilishwa na Katibu wa Rais Ngusa Samike kwa Sheikh Mkuu wa Wilaya Suleiman Abdallah Matitu.

Pamoja na kukabidhi fedha hizo, Rais Magufuli amewapongeza na kuwashukuru watu wote waliounga mkono na wanaoendelea kuunga mkono uchangiaji wa ujenzi wa Msikiti mpya na wa kisasa wa Wilaya ya Chamwino.

Rais Magufuli pia amesema kuwa Msikiti huo utajengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na ujenzi wake utaanza wiki hii na kuongeza kuwa watu mbalimbali wameguswa bila kujali madhehebu ya Dini waliyonayo na kwamba hiyo ni uthibitisho wa umoja na mshikamano walionao Watanzania.

Jana Agosti 23, 2020, wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Emmaculata iliyopo Chamwino, Rais Magufuli alitoa rai kwa waumini kuchangia ujenzi wa msikiti huo kwa lengo la kuhakikisha Makao Makuu ya nchi yanazungukwa na uwepo wa Mungu, ambapo kwa siku ya jana alifanikiwa kukusanya zaidi ya Milioni 40.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad