First Eleven Simba, Yanga ni Balaa



HIVI ushavuta picha mechi ya Simba na Yanga ya msimu ujao itakuwaje? Kama bado hujafikiria kwa namna itakavyokuwa basi tambua kwamba zitakapokutana timu hizo moto utawaka kutokana na aina ya usajili ambao wamefanya.

Yanga imeamua kuingia sokoni na kushusha majembe ya ukweli wakiwa wanashirikiana na wadhamini wao, Kampuni ya GSM ambayo imepanga kufanya makubwa ndani ya kikosi hicho.

Hadi sasa Yanga imeshasajili nyota kadhaa ambao wamewapa mikataba na kuwatambulisha rasmi huku pia kukiwa na nyota ambao wanaendelea kuzungumza nao na kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 31, basi watakuwa wameshawatambulisha.


Wakati Yanga wakiwa wanafanya usajili huo, wapinzani wao Simba nao wanafanya mambo yao kimyakimya ambapo usajili wao mkubwa ambao wameufanya hadi sasa ni wa winga Mghana, Bernard Morisson aliyetokea Yanga na Mcongo Papy Tshishimbi naye yupo njiani.


Baada ya mambo ya usajili, Championi Jumatatu linakupa taswira ya namna vikosi hivyo vitakavyokuwa wakati wakikutana na kwenye mechi zao nyingine za ligi.


Kwa upande wa Simba, kipa Aishi Manula bado ana nafasi ya kucheza, walinzi wanatarajiwa kuwa David Kameta ‘Duchu’ (beki wa kulia) au Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (beki wa kushoto) huku mabeki wa kati wakiwa Pascal Wawa na Mkenya Joash Onyango anayetokea Gor Mahia ambaye inatajwa usajili wake upo mwishoni kukamilika.

Kwa upande wa viungo watasimama; Papy Tshishimbi ambaye analetwa kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo mkabaji na Mbrazili, Gerson Fraga, viun go wa mbele ni Clatous Chama, Luis Miquissone raia wa Msumbiji na Bernard Morrison huku straika akiwa ni John Bocco au Meddie Kagere.

Lakini kutakuwa na ongezeko la mshambuliaji Charles Ilanfya aliyesajiliwa kutoka KMC na straika Mzambia anayetoka Lusaka Dynamo.

Kwa upande wa Yanga, langoni atasimama Metacha Mnata, beki mpya Kibwana Shomari aliyetua akitokea Mtibwa Sugar atapewa nafasi ya mlinzi wa kulia. Kushoto atacheza Mnyarwanda Erick Rutanga aliyesajiliwa akitokea Rayon Sports.

Pia kwenye kikosi hicho, kutakuwa na pacha mpya ya Bakari Mwamnyeto ambaye ametokea Coastal Union pamoja na Mghana Lamine Moro huku Mkongomani Tonombe Mukoko akiwa kwenye eneo la kiungo mkabaji.

Si ajabu pia kwenye kikosi hicho kuwemo kwa kiungo Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ ambaye muda wowote dili lake linaweza kukamilika baada ya kuomba kuondoka Azam FC, sasa yeye atakacheza na Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika eneo la kiungo cha timu hiyo.

Straika raia wa Bukina Faso, Yacouba Songne anayeichezea Asanté Kotoko ya Ghana ataanza kwenye eneo la ushambuliaji sambamba na Farid Mussa (ambaye naye yuko mbioni dili lake kukamilika klabuni hapo) huku Mkongo mwingine Tuisila Kisinda akiongeza nguvu kwenye eneo hilo la ushambuliaji.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad