Habari Njema Kuhusu CORONA, Urusi Kutumia Watu 40,000 Majaribio Chanjo ya Corona



Wanaounga mkono mradi wa Urusi wa chanjo ya virusi vya corona wanasema majaribio ya chanjo hiyo ya kwanza nchini humo yatafanyiwa zaidi ya watu 40,000 yatakapoanza wiki ijayo.

 Inadaiwa kwamba majaribio hayo yatasimamiwa na shirika la nje ya Urusi. Hii ndio taarifa ya kwanza kutolewa na watengenezaje wake ambao wanataka kuondoa wasiwasi kutoka kwa baadhi ya wanasayansi wanaohofia ukosefu wa data kutoka kwa serikali ya Urusi kuhusiana na chanjo hiyo kufikia sasa.

Chanjo hiyo kwa jina "Sputnik V" imesifiwa na serikali ya Urusi na wanasayansi nchini humo kufuatia miezi miwili ya majaribio kwa binadamu. Matokeo ya majaribio hayo lakini hayajawekwa wazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad