KUMEKUWA na kasumba ambayo inawaandama sana mastaa wa muziki hapa Bongo.
Hii imesababisha baadhi ya mastaa waponzwe na warembo hao, kwani watu wamekuwa wakiona tu picha za video wakiwa pamoja, basi wanajiongeza kwa kusema walikuwa wapenzi.
Japo nyingine zinaweza kuwa ni uvumi lakini wapo wanamuziki waliofanya kweli kwa video vixen hao.
Makala haya yanakuletea orodha ya wanamuziki wakubwa ambao wamewahi kuhusishwa katika ishu hizo:
DIAMOND-HAMISA
Mwanamuziki mkubwa Afrika Mashariki, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi mwenza wake Hamisa Mobeto ambaye alionekana katika video mbili ya Nataka Kulewa na Salome.
Licha ya kuwa video vixen, wawili hao walikuwa wapenzi na kufanikiwa kuzaa mtoto mmoja.
DIAMOND-TUNDA
Anastazia Sebastian almaarufu kama Tunda, aliwahi kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz ikiwa ni baada ya kuonekana katika wimbo wa Salome.
Japo wawili hao walificha, habari zikasambaa baada ya video yao kuvuja.
KIBA- HAMISA
Mfalme wa Bongo Fleva na Bosi wa Lebo ya King’s Music Records, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, baada ya kutoa ngoma ya Dodo na video vixen akiwa mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Kukazagaa habari kuwa wawili hao wametoka kimapenzi na walilala hoteli moja, lakini hata hivyo ilibainika hazikuwa na ukweli na wenyewe walikanusha.
KIBA- TANASHA
Ali Kiba ‘King Kiba’, aliwahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki kutoka Nairobi, Kenya Tanasha Donna ambaye pia ni mzazi mwenzake na bosi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kiba na Tanasha walikutana katika ngoma ya Nagharamia ambayo Tanasha alikuwa ni Video Vixen katika ngoma hiyo, hata hivyo wawili hao hawakuwa wapenzi.
RAYVANNY – NANA
Memba kunako Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa almaarufu kama Rayvanny, aliwahi kuhusishwa na skendo ya kutoka na mrembo anayekwenda kwa jina la Nana.
Nana alishiriki katika ngoma ya I Love You ya Rayvanny na baada ya hapo zikasambaa tetesi kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini hata hivyo hakukuwa na ukweli wowote.
KIBA – GIGY MONEY
King Kiba aliwahi kutajwa kuwa ana-date na Gigy Money kipindi akiwa video vixen kabla ya kuzamia kwenye muziki.
Gigy aliwahi kukiri kuwa Kiba ni mwanaume mzuri na ana mvuto na aliwahi kumuumiza katika mapenzi kipindi wako pamoja.
Kiba hakuwahi kukiri kuwa wapenzi na Gigy.
Gigy pia aliwahi kumtamani Mondi na kusema kuwa akiomba kulala naye, lazima atafanya hivyo kwani anamkubali sana staa huyo na bosi wa lebo ya Wasafi.
HARMONIZE- NICOLE
Staa wa ngoma ya Wife na Bosi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, Rajab Abdul ‘Harmonize’ aliwahi kuhusishwa na skendo ya kutoka na mrembo mwenye zigo la kuvunja chaga Nicole Jowberry.
Nicole alishiriki katika ngoma ya Bedroom na zikasambaa tetesi kuwa na uhusiano wa kimapenzi, japo wote wawili walikanusha skendo hiyo.
YOUNG DEE-AMBER LULU
Staa wa Hip Hop Bongo, David Genzi ‘Young D’, aliwahi kutajwa kutoka na aliyekuwa video vixen wake katika ngoma ya Bongo Bahati Mbaya, mwanadada Lulu Eugen ‘Amber Lulu’.
Young Dee anatajwa kuwa aliendelea kuwa na uhusiano na Amber Lulu kwa muda mfupi kabla ya kubwagana bila sababu kujulikana.
MAKALA:HAPPYNESS MASUNGA