HESLB yatoa siku kumi kwa wanafunzi vyuo vikuu




Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) imeongeza Bajeti yake ya mikopo hadi shilingi bilioni 464 kwa mwaka huu kutoka shilingi bilioni 450 mwaka wa jana ampapo hadi kufikia jana tayari wanafunzi takribani elfu sabini na moja mia nane wameshamilisha usajili wa maombi ya mikopo.


Akitoa taarifa ya hali ya maombi ilivyo kwa sasa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Abdulrazak Badru amesema hadi aasa zaidi ya asilimia 84 ya wanafunzi walioomba mikopo wamekamilisha taratibu zote na ili kukamilisha usajili kwa waliobakia bodi ya mikopo imeongeza muda hadi Septemba 10,2020 ili wanafunzi waliopo kwenye mchakato wakamilishe mara moja.


"Kwa Sasa Bodi imekuwa ikitoa Elimu Nchini nzima Ambapo mpaka Sasa tayari mikoa 14 imefikiwa ili kuwafundisha wanafunzi namna ya kujaza fomu za maombi kwa usahihi huku tukikumbusha umuhimu wa kulipa mkopo endapo ulikopeshwa ili wengine pia wakope ingawa kwa Sasa Kasi ya urejeshaji ni kubwa" AbdulRazak Badru Mtendaji Mkuu Bodi ya Mikopo HESLB.


Kwa upande mwingine bodi hiyo inashirikiana na shirika la posta pamoja na wakala wa usajili vizazi na vifo nchini (RITA) ili kuhakikisha kwa pamoja wanakamilisha mchakato wa uhakiki wa vyeti na kutumwa kwa usahihi.


"Sisi Kama wakala wa usajili wa vyeti vya uzazi na Vifo tunawajibu wa kuhakiki vyeti vyote katika  maombi yote  wanafunzi waliyotuma Ambapo Hadi Jana agosti 30,2020 tayari vyeti vya kuzaliwa zaidi ya elfu 97700 tayari vilikwisha hakikiwa"Josepat kimaro-Mkuu wa kitengo Cha Habari  RITA.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad