Hezbollah yatangaza kudungua ndege isiokuwa na rubani ya jeshi la Israel



Hezbollah nchini Lebanon yataganza kudungua ndege isiokuwa na rubani ya jeshi la Israel  ikifahamisha kwamba ndege hiyo ilivuka mipaka ya anga ya kimataifa na kuingia katika anga  la Lebanon.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Kusini mwa Lebanon mpakani na Israel.

Ndege hiyo isiokuwa na rubani  imedunguliwa Agosti  22 katika anga la Aita al Shaab katika mji wa Nabatiah Kusini mwa Lebanon.

Taarifa iliotolewa na chama cha Hezbollah  imefahamisha kwamba  mabaki ya ndege hiyo yapo mikononi mwa  mwake.

Hakuna  taarifa  ambayo imetolewa na  Israel kuhusu tukio hilo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad