Wakati nikiendelea kukimbia kwa mbele kama nusu Kilometa hivi nikamuona mtu mwingine nae akikimbia. Bila shaka alikua akikimbia taratibu kuliko mimi. Hapo hapo nikajiambia nikimbie mpaka nimfikie na kumpita. Nilikimbia kwa kasi ilimradi tu nimfikie na kumpita.
Baada ya dakika chache nikawa nimebakiwa na kama mita 100 hivi nimfikie, mara akachepuka kushoto mwa barabara. Nikajiambia kuwa nia yangu nataka nimpite hivyo alivochepuka na mimi nikamuungia na kuendelea kumfuata.
Nikiwa nimekaribia kumfikia nikazidisha speed kama Usain Bolt amefikia utepe wa mwisho wa mashindano ya olimpic. Moyoni mwangu nikafarijika sana kumpita, na nilifurahi mno, nisijue kuwa mwenzangu hata hakuwa na wazo kuwa tulikuwa tukishindana. Hili lilikuwa wazo langu binafsi.
Baada ya kumpita na kwenda umbali mrefu kidogo mara nikahisi kama nimepotea na sijui ni wapi ninaelekea. Kuangalia saa ilikuwa ni saa moja na dakika 45 na saa moja kamili nilikuwa na appointment muhimu sana ya pesa. Hivyo ikanibidi kuanza kurudi nilikotoka.
Nikiwa nimepoteza muda na mpaka nafika nyumbani hakukuwa na appointment tena maana nilipoteza muda mwingi. Hivyo na pesa nikaikosa pia.
Haya ndio yanatokea katika maisha yetu ya kila siku pale tunapoweka mashindano na wafanyakazi wenzetu, majirani zetu, marafiki, na familia ili tuwaonyeshe kuwa tuna mafanikio au wa muhimu kuliko wao? Tunatumia nguvu nyingi pamoja na muda mwingi kuwafukuzia na imefika hatua mpaka tukasahau njia zetu.
Tumejisahau kuwa kila mmoja ana mwisho wake wa tofauti. Tatizo la mashindano yasiyo na tija ni kuwa huwa hayana mwisho.
Katika Maisha lazima kutakuwa mtu ambaye yupo juu au mbele yako hata ufanyeje.
Lazima atakuwepo mtu ambaye ana hela kuzidi zako, lazima atakuwepo mtu ambaye ana elimu kukuzidi wewe pamoja na ukoo wenu wote, lazima atakuwepo mtu ambae ana kazi nzuri kuzidi yako, gari zuri kuzidi lako, pesa nyingi Bank kuzidi zako, mke mzuri kuzidi wako, mume mzuri kuzidi wako, watoto wenye tabia nzuri kuzidi wako na kadhalika.
Hata ufanyeje hauwezi kuwa juu au mbele kuliko wote. Lakini kumbuka unaweza kuwa bora sana (the best) kama utaamua kuwa wewe kama wewe. Watu wengine imefika hatua wamekosa hadi raha kwa kuwa wamekua wakiangalia sana majirani zao jinsi wanavyoishi, wanavyokula, magari wanayoendesha, utajiri wao n.k. Shukuru Mungu alichokupa, fanya kazi kwa bidii ukiangalia ni nini mahitaji yako, usinunue kitu ilimradi tu kwa kuwa jirani yako au rafiki yako anacho, kwa kuwa itafika wakati itakibidi uuze vitu ambavyo ni vya muhimu.
Ishi maisha ya furaha, vaa vizuri kula vizuri. Relax hakuna mashindano katika hatima ya mtu.
Alichokupangia Mungu utakipata tu. Hata kicheleweshwe vipi utakipata tu. Vuta subira huku ukijibidiisha.
Kimbia mbio zako binafsi na watakie wengine kila la kheri!
SHARE na Marafiki zako kama Unakubaliana nami
*Your Dream Our Plan*