Hizi Hapa Dalili za Kuwa Mtoto Wako ana Akili Kuliko za Kawaida "Genius"


Wazazi wengi hujivunia watoto wao walio werevu kutokana na sifa wanazopata kwa sababu ya weledi wao. Hii ni kutokana kuwa Wengi hupenda watoto wawe werevu na wako radhi kufanya chochote kuimarisha kitu kizuri katika maisha ya watoto wao.

Werevu wa mtoto unaweza kutambuliwa akiwa mdogo kisha kukuzwa kwa b; ya kumfaidi atakapokuwa mtu mzima.

Udaku Special Blog imekuorodheshea ishara, vidokezo na vitendo vitakavyokuonyesha kuwa mtoto wako ni mwerevu sana na hizi hapa ni njia 11 za kutambua iwapo mtoto wako ni ‘Genius’.

1. Kutambua Muundo na Fomu Akiwa Mchanga

Kuna watoto ambao huwa na uwezo wa kutambua muundo na fomu wakiwa wachanga. Hali hiyo inaweza kugunduliwa kutokana na jinsi mtoto anavyotumia vifaa vya michezo vya watoto, kadi, kifaa cha michezo cha ‘brick’ miongoni mwa michezo mingine.

Ikiwa mtoto anaweza kutambua na kuambatanisha muundo na fomu, basi hiyo ni ishara tosha kuwa mtoto huyo ni mwerevu sana. Kumbuka, kuna watu wazima ambao wanatatizwa sana kuambatanisha miundo na fomu!!.

2. Ari Ya Kujua Mengi Duniani

Umewahi kuulizwa na mtoto akiwa mdogo, Mfano swali kwamba “Watoto hutokea wapi?”

Kuna watoto wanaouliza na kukata kujua mambo yanayowazingira, kwa mfano chakula chao, vitu vyao vya kucheza na kadhalika, lakini mtoto mwerevu hutaka kujua jinsi kila kitu kinavyotokea na kwa nini.

Watoto werevu huwazonga wazazi wao na maswali mengi ambayo watu hudhani ni rahisi kujibu mpaka pale wanaposhindwa kupata majibu sahihi. Mtoto ambaye hutaka kujua mambo kwa kina anaonyesha kuwa yeye ni mwerevu.

03. Kujua Lugha Mapema

Watoto wanaopata maendeleo makubwa wakiwa wachanga kama kuweza kuzungumza lugha ya mama au Kiswahili vizuri ni ishara kuwa ni werevu.

Watoto hao huwa na ujuzi mkubwa wa lugha unaozidi ule wa umri wao na wanaweza kubuni sentensi zilizoboreka. Kwenye masomo ya isimu, weledi wa lugha humsaidia mtu kuwa na mawazo pana, hali inayodhibitisha kuwa ikiwa mtoto wako ameimarika kwa lugha akiwa mchanga, basi yeye ni mwerevu.

04. Kujua Maswali Ya Kitu Fulani Kwa Undani

Watoto wanaojua mambo kuhusu mada fulani kwa undani wanaonyesha kuwa ni werevu, kwa mfano mtoto mdogo kwa jina Aithamu Masoud kutoka Bukoba, aliyesisimua mitandao kwa jinsi alivyowajua marais wote wa bara la Afrika na Mawaziri ni ishara kuwa ni mwerevu.

Pia mtoto ambaye hajatimiza umri wa miaka 11 ambaye ana weledi wa mada zinazosomwa na kuangaziwa na watu wazima ni ishara kuwa yeye ni mwerevu.

05. Sifa za Uongozi

Mzazi anaweza kugundua sifa za uongozi kwa mtoto wake kutokana na jinsi anavyowapanga watoto wenzake wanapocheza au wakiwa mahali, kuandaa vitu vyake kama vitabu kwa utaratibu na ujasiri wake kwa yale anayoyafanya.

Watoto ambao huonekana wakiwa na sifa za uongozi wana nafasi ya kuwa viongozi siku za usoni na bila shaka sifa hizo ni ishara ya mtoto mwerevu.

06. Wana malengo, Uamuzi na Misimamo Dhabiti

Watoto wadogo wanaweza kushawishiwa kwa urahisi kufanya lolote, lakini mtoto asiyekubali kitu chochote anachoambiwa kwa kuamini kuwa sio nzuri kwake ni mwerevu, kwa mfano wao hukataa kushawishiwa kufanya makosa shuleni.

Watoto wanaoonyesha kufuata na kutimiza malengo na uamuzi wao bila ya kubabaika ni watoto werevu.

07. Wanapendelea Kukaa na Watu Wazima Zaidi Ya Watoto wa Umri Wao

Kuna watoto ambao utawapata kwenye vikao vya watu wazima kila mara. Wakati mwingine, wazazi wao hulazimika kuwafukuza ili waweze kusemezana mambo ya watu wazima. Hii ni ishara kuwa mtoto huyo ni mwerevu na utamwona akiendeleza mazungumzo na mtu mzima katika hali ya wastani.

Mtoto kama huyo anastahili kusaidiwa kuwapata marafiki wa umri tofauti ili kuimarisha hali yake kimawazo. Watoto hao wakati mwingi hawafurahishwi na kazi zao za darasani kwa kuwa kwao ni rahisi sana.

08. Hufanya Vizuri Masomoni

Wataalamu wa teknolojia mpya za kimatibabu zinazoangazia jeni wamedhibitisha kuwa ikiwa mtoto anafanya vizuri kwenye masomo yake, basi huenda mtoto huyo ni mwerevu sana. Uwezo wa mtoto wa kufanya vizuri katika somo la hesabu na somo la lugha ni ishara tosha kuwa yeye ni mwerevu.

9. Wana Uhalisia Wao

Watoto werevu wanakubali mawazo ya watu wengine, lakini wana mbinu na mawazo yao kuhusu jambo fulani au kuhusu jinsi ya kukifanya kitu fulani.

Watoto werevu huwa na ari na bidii ya kutafuta njia nyingine ya kutatua jambo fulani. Utamsikia mtoto akimuuliza mwalimu au wazazi wake, “Ni njia nyingine ipi tunayoweza kutumia kutatua jambo hiyo/hesabu hiyo?” Hiyo ni ishara kuwa mtoto huyo ni mwerevu.

10. Wana Udhaifu Kama Binadamu Wengine

Mtoto mwerevu atakuwa na udhaifu kwa sababu kadhaa. Anaweza kuwa na udhaifu kwa jambo fulani kwa kuwa yeye ni mtoto na kuna mambo ambayo atakosea.

Yawezekana kuwa mwanao ni gwiji kwenye somo la hesabu, lakini somo la sayansi linamtatiza. Watoto werevu wanaweza kuwa udhaifu wa kutojali, kutatizika kiakili na kukosa ujuzi wa kawaida.

11. Wanapenda Kusoma

Watoto werevu hupenda kusoma na hujifunza kusoma haraka kuwalika wenzao walio na umri sawa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad