Hizi ndizo gharama unazopaswa kuzifahamu kabla ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi


Kabla ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi zipo gharama za msingi unazopaswa kuzifahamu kabla ya kuingia katika mahusiano hayo. Watu wengi wamekuwa hawadumu katika mahusiano yao ya kimapenzi wanayoaanzisha mara kwa mara hii ni kwa sababu watu hao wamekuwa hawajui lengo pamoja na gharama wanazotakiwa kuzifahamu kabla ya kuingia katika mahusiano hayo ya kimapenzi.

Zifutazo ndizo gharama za msingi  unazotakiwa kuzifahamu  kabla ya kuingia katika mauhusiano ya kimapenzi:

1. Mahusiano yanahitaji gharama ya Muda.
Ukweli ambao upo wazi na ambao hauna kipingamizi ni kwamba kabla ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi unatakiwa kuelewa kuwa muda ni jambo la msingi sana litakalokusaidia mahusiano yenu yaweze kudumu. Kama bado unathamini muda wa mambo yako sana kuliko kitu kingine, tulia usiingie kwa mahusiano utavunja mahusiano ndani ya miezi michache. Mahusiano yanahitaji muda wa mwingi wa kuweza kujua mambo mbalimbali kutoka kwa mwenzako unaye anza safari  ya kimahusiano.

Ukiona unahisi kero kupotezewa muda na mwenzako iwe kwa mazungumzo ,kutoka out, kupumzika, kupanga, na kufanya shughuli alokuhusisha,jua wewe bado kisaikolojia ni mdogo (mtoto) hujakomaa huruhusiwi kuingia katika mahusiano maana mtapigizana kelele na mwenzako mwisho wa siku ni lazima mtaachana.

2. Gharama ya Kuomba Samahani.
Unaweza kuona ni jambo dogo kumbe hii ni gharama kubwa inayoshinda wengi na kupelekea mpasuko na mtafuruko katika  mahusiano. Kama bado kinywa chako ni kizito kusema nisamehe mke wangu, mme wangu, mchumba wangu, usianzishe mahusiano hayo kwani  hayatadumu.

3. Gharama ya Kupenda.
Upendo una gharama zake zisizo kuwa na kikomo, hivyo unashauriwa ya kwamba kabla ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi ni lazima uelewe gharama za kupenda. Gharama za kupenda ni kama vile kuwa subira, kuwa muaminifu, kujali,  kufurahi pamoja na mwenza wako pamoja na kuwa ya roho ya kumsifia mwenza wako kila wakati. Hivyo kama utashindwa kuvitambua vitu hivyo unashauriwa kutoingia katika mahusiano ya kimapenzi.

4.  Gharama ya kuheshimu na kutii.
Kama unaona huwezi kuwa msikivu, kufuata na kutii kwa mwenzako kwa sasa unashauriwa usifanye haraka kuingia katika mahusnao ya kimapenzi jipange kwanza uandae saikolojia yako, kuongozwa kwa kufuata mwenza wako wako anataka ufanye nini ili msikwazane.

5. Gharama ya Kuachana na wazazi,ndugu na jamaa.
Unapotaka kuingia ulimwengu wa malavidavi, kuna gharama kubwa ambayo unatakiwa kuifahamu ambayo kimsingi wakati mwingine itautesa  sana moyo wako kwa kiwango cha hali ya juu sana, na gharama hii si nyingine bali gharama ya kuachana na ndugu na jamaa ambao uliwakuwa nao karibu.

Hivyo kama unataka kuingia katika mahusiano ya kimapenzi akili yako ni lazima uwaze juu ya kuishi kutoka na mazingira ya namna hii ya kuachana na ndugu zako wa karibu ambao mlikuwa mnapendana kwa dhati.

Hivyo kila wakati kama unataka  kudumu katika mahusiano yako ya kimapenzi unatakiwa kufahamu gharama hizo za msingi zitakazokufanya uweze kudumu katika ya kimapenzi.

Na. Benson Chonya.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad