INDIA: Watu 10 wapoteza maisha kwa kunywa vitakasa mikono kisa pombe kupigwa marufuku



Watu 10 wamekufa kwa kunywa kitakasa mikono kilichochanganywa kwa pombe baada ya uuzaji pombe kupigwa marafuku katika kijiji kilichopo jimbo la Andhra Pradesh nchini India.




Kijiji cha Kurichedu kimewekewa hatua ya kutotoka nje kama njia moja ya kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.


Polisi wa eneo la Siddharth Kaushal alisema kuwa watu waliokufa walikuwa wamechanganya kitakasa mikono na vinywaji vitamu mfano wa soda.


Watu hao walikuwa waraibu wa pombe, aliongeza, walikuwa wameanza kunywa mchangayiko huo siku 10 kabla ya kufa.


“Tunachunguza ikiwa kitakasa mkono kilikuwa na sumu nyengine yoyote,” Bwana Kaushal amewaarifu wanahabari.


Aliongeza kwamba wametuma sampuli za vitakasa mkono vingine kufanyiwa uchunguzi.


 


“Watu wengine ambao walikuwa waraibu wa pombe kupindukia wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha vitakasa mikono,” amezungumza na shirika la habari la Reuters.


“Sasa hivi pombe haipatikani kwasababu ya hatua ya kutotoka nje iliyowekwa, lakini vitakasa mikono vinapatikana kwa urahisi.”


Serikali ya India imefungua biashara nyingine nyingi kuzuia kuporomoka kabisa kwa uchumi


Mapema wiki hii ilitangaza kwamba vituo vya yoga na mazoezi ya viungo vitafunguliwa tena na kwamba masharti dhidi ya usafiri wa mizigo na watu yataondolewa.


Hata hivyo majimbo mengi bado yanaendeleza hatua za kutotoka nje huku maambukizi yakizidi kuongezeka.


Maaambukizi ya virusi vya corona katika jimbo la Andhra Pradesh, kusini mwa India yameongezeka mara tisa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad