Jay Z Kupitia ROC Nation Watangaza Kuanzisha Shule ya Muziki na Burudani
0
August 06, 2020
"I'm Not a Businessman. I'm a Business, Man." rapa na mfanyabiashara tajiri Jay-Z ameendelea kuutendea haki msemo wake huo.
Jana zilitoka taarifa kwamba kampuni yake ya Roc Nation imepanga kukuza na kukiendeleza kiwanda cha muziki hasa katika mji wa Brooklyn ambao Jay-Z anatokea. Roc Nation kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Long Island University (LIU) wametangaza ushirikiano wa kuanzisha shule itakayotoa elimu kuhusu Muziki, Michezo na Burudani.
Shule hiyo (Roc Nation School of Music, Sports & Entertainment) itaanza kupokea wanafunzi wa muhula wa kwanza kuanzia mwaka 2021 katika Cumpus za chuo cha LIU mjini Brooklyn Marekani. Lengo ni kuimarisha uwezo wa vijana katika nyanja hizo tatu ili kuwa wana mabadiliko kwenye masuala ya menejimenti katika Muziki, Michezo na Burudani.
Tags