Jennifer Lopez atangaza kufungua kampuni ya urembo



Mwanamzuki na Muigizaji Mkongwe Jennifer Lopez anafata nyayo za Rihanna, Kylie Jenner, Ariana Grande, Lady Gaga na Jessica Alba, ametangaza kufungua kampuni ya Urembo 'JLO Beauty'



Siku ya jumatatu mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 51 alitangaza kupitia Instagram kuwa anafungua kampuni yake ambayo itakuwa inatengeneza bidhaa za urembo, Uzinduzi wa kampuni hiyo unakuja miaka miwili baada ya kudokeza ujio wa bidhaa zake binafsi za urembo.




Rihanna na Kylie Jenner ni kati ya mastaa wanaotajwa kuingiza kipato kikubwa cha pesa kupitia makampuni ya Urembo, Kylie Jenner anakaribia utajiri wa dola Billioni 1 huku Rihanna akiendelea kutesa kama mwanamuziki wa kike tajiri zaidi mwaka wa nne bila ya kuachia album huku chanzo kikubwa kikiwa ni kampuni yake ya urembo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad