Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro Limewakata Watuhumiwa 12 Waliomfanyia Lissu Vurugu



Jeshi la Polisi mkoani kilimanjaro limewakata watuhumiwa 12 wanaodaiwa kufanya vurugu za kushambulia kwa mawe, mkutano wa mgombea wa Kiti cha Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu Wilayani Hai Mkoani humo wakati akiendelea na zoezi lake la kutafuta wadhamini. 


Taarifa hiyo imetolewa hii leo Agosti 23, 2020 na Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Emmanuel Lukula na kusema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 14 mwaka huu, ambapo katika mahojiano yao na vijana hao wamedai kuwa kulikuwa na mtu nyuma yao ambaye amekimbia. 


"Tumetumia sana intelejensia ya Polisi ili kuwabaini hao watu waliofanya kitendo hicho cha aibu kubwa tumefanikiwa kuwapata 12, wengine tumewakamatia Arusha wanasema baada ya hilo tukio waliona kama wangerudi majumbani mwao wangekamatwa, tumewafuatilia kwa muda mrefu lakini tumeona tuwafuate walipo, mbaya zaidi wanatueleza kuwa kuna mtu aliyekuwepo nyuma yao na amekimbia" amesema Kamanda Lukula. 


Aidha Kamanda Lukula ametoa angalizo na onyo kwa vijana, watakaotumika kisiasa kufanya vurugu katika mikutano mbalimbali ya vyama vya siasa mkoani kilimanjaro na kuwataka kuzingatia sheria za nchi kwa kufanya shughuli halali bila kutumiwa katika matukio ya kihalifu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad