Jinsi ya Kujiokoa Unapokua Umedumbukia kwenye Bahari


Mwanamke mmoja muingereza ameokolewa baada ya kukaa saa kumi kwenye maji katika bahari iliyopo fukwe za Croatia baada ya kuanguka kutoka upande wa nyuma wa meli.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 alikuwa peke yake na sehemu aliyoangukia ilikuwa ni maili 60 kutoka kwenye fukwe wakati alipookolea kupelekwa hospitali.

Maelezo zaidi kuhusu kupona kwake kwa kushangaza bado yanaendelea kufuatiliwa.

Lakini ukikutana na hali kama hiyo ni nini ambacho unaweza kukifanya ili kikusaidie uweze kujiokoa?

Kulikuwa sababu kadhaa ambazo zilimsaidia kuokolewa Kay Longstaff.

Mtaalamu wa uokozi katika maji ,Simon Jinks alisema mwanamke huyo alizama mita tatu au nne katika maji mara baada ya kuanguka na hiyo ilimsaidia kutovutwa na meli.

Kwenye maji kuna mawimbi ambayo yanaweza kukusukuma lakini vilevile inategemea na mwendo wa meli lakini vilevile inategemea na bahati ya mtu.

Vilevile inawezekana upepo au mawimbi yalivyokuwa yanavuma katika upande wa meli hiyo .

Sababu nyingine ambayo zinaweza kumfanya mtu apone ni joto la maji ,kwa kukadiria inawezeana alizama kwenye maji ambayo yalikuwa na nyuzi joto28 au 29,au yalikuwa na joto zaidi ya kwenye bwawa la kuogelea,allisema hivyo mtaalamu wa mazingira ya ukoaji katika maji .

Mtu anaweza kupona kwa saa moja katika maji yenye nyuzi joto 5,masaa mawili kwa nyuzi joto kumi na saa sita kwa nyuzi joto 15 lakini kama joto ni kali zaidi ya nyuzi joto 20 basi inawezekana mtu kuweza kupona kwa saa zipatazo 25.

Binadamu wanaweza kuwa kwenye maji baridi kama joto lake ni dogo ,hii ikiwa inamaanisha kwamba inaweza kumpa uwezo wa kupumua na kuelea kwenye maji bila kuzama.

Na kama joto la mwili litapanda basi mtu anaweza kuchoka kwa haraka,kuchanganyikiwa au kufadhaika.

Kama angezama katika bahari iliyopo karibu na Uingereza basi angekuwa kwenye maji yenye nyuzi joto 12 na 15 ambao ni ubaridi wa kutosha wa kufanya maji yamshtue mtu.

Jaribu kuelea

Kwa mujibu wa muongozo wa njia za kujiokoa ambacho kiliandikwa na wavuvi kutoka Irish ,namna nzuri ya kuweza kujiokoa ni kutokuogea badala yake inabidi uelee tu katika maji wakati magoti yako yakiwa umeyanyanyua mpaka kwenye kifua chako.

Hivyo inawezekana mwanamke huyo alitulia na akaweza kuwa anaelea na kuogelea lakini alibaki katika eneo lile lile aliloangukia,


Hakuweza kuwa amepigwa na mawimbi kwa wakati wote bila shaka ndio maana hakuweza kuzama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad