Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akila Mhindi wa Kuchoma katika eneo la Dumila Darajani wakati aliposimama kuzungumza na wafanyabiashara hao wadogowadogo akiwa njiani kuelekea Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesimama na kuwasalimia wafanyabiashara wa mazao eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro na kuwaahidi kuwapatia shilingi Milioni mia moja kwa ajili ya Ujenzi wa mabanda ya kisasa.
Magufuli ametoa ahadi hiyo baada ya wafanyabiashara hao kumuomba waongezewe eneo hilo lililopo kando ya Barabara iendayo Dodoma.
Aidha, Rais Magufuli amenunua muhindi kwa vijana wachoma mahindi wa eneo hilo la Dumila aliposimama kuwasalimia wafanyabiashara hao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Dumila Darajani mkoani Morogoro wakati akielekea mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Mhindi wa Kuchoma kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Mhindi wa Kuchoma kutoka kwa mfanyabiashara mdogo katika eneo la Dumila Darajani wakati akielekea mkoani Dodoma.
Wafanyabiashara wa Dumila Darajani wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kusimama katika eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma.
Rais Dkt. John Magufuli akifurahia muhindi alionunua eneo la Dumila aliposimama kuwasalimia wafanya biashara wa mazao na mahindi ya kuchoma walio kando ya barabara eneo la Dumila mkoani Morogoro.