Juhudi za uokozi zaendelea Beirut, idadi ya vifo yafikia 100




Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kuwatafuta watu waliofukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka, siku moja baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika katika bandari ya Beirut na kuwauwa karibu watu 100. 


Shirika la Msalaba Mwekundu la Lebanon limesema karibu watu 4,000 wamejeruhiwa na huenda idadi ya vifo ikaongezeka. 


Afisa mmoja wa ulinzi wa kiraia amesema bado wanawatafuta karibu watu 100 waliofukiwa kwenye vifusi, hasa karibu na bandari ya Beirut. 


Walebanon wameamka leo na kushuhudia uharibifu mkubwa uliotokea katika bandari hiyo pamoja na maeneo ya karibu katikati mwa mji huo mkuu. 


Wafanyakazi wanaendelea kuondoa vifusi ili kufungua barabara na kukarabati maeneo yaliyoharibiwa. Baraza la Mawaziri la Lebanon linatarajiwa kufanya kikao cha dharura leo baada ya Baraza Kuu la Ulinzi la Lebanon kuitangaza Beirut kuwa eneo la janga na kupendekeza hali ya hatari kwa wiki mbili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad