Kenya Kupokea Chanjo ya COVID19 Kutoka Urusi, Balozi wa Urusi Athibitisha



Wiki moja tu iliyopita Rais wa Urusi Vladimir Putin alithibitisha kuwa nchi yake ilifanikiwa kutoa chanjo ya COVID19 na kuidhinishwa rasmi kwa matumizi.

Kulingana na kiongozi huyo, chanjo hiyo ni shwari na kuwa bintiye ni kati ya watu wa kwanza waliopewa

Kenya huenda ikawa kati ya nchi za kwanza kupokea na kutumia chanjo hiyo, hii ni baada ya balozi wa Urusi nchini Kenya Amb Dmitry Maksimycjev kuthibitisha kauli hiyo.

Akihojiwa na kituo cha runinga, balozi huyo alisisitizia kauli ya Putin kuhusu uhalali wa chanjo hiyo na kuthibitisha kuwa haina madhara yoyote.


Amerika ilitofautiana na Urusi kuhusu uhalali wa chanjo yao. Picha: Hisani.

Hatua hii inajiri wiki moja tu baada ya wizara ya afya kuwaahidi Wakenya kufanya mazungumzo na serikali ya Urusi kuhusu kuagiza chanjo hiyo.

Urusi ilishangaza ulimwengu kwa kutangaza kupata chanjo ya COVID19 mbele ya mataifa mengine yaliyoendelea kama vile Amerika, Japan na Uchina.

Amerika imetofautiana vikali na Urusi kuhusu chanjo hiyo, baadhi ya maafisa wa afya wakieleza kuwa hawawezi kutumia chanjo hiyo hata kwa nyani.

Licha ya hayo yote,Rais wa Urusi Vladimiru Putin kwa uapande wake amethibitisha kuwa chanjo hiyo ipo shwari na hata kukiri kuwa bintiye ni kati ya watu wa kwanza waliopewa chanjo hiyo.

Uchina na Japan zimeeleza kuwa wako katika hatua ya mwisho katika kubuni chanjo dhidi ya virusi hivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad