Kesi Za Uchaguzi Kumalizika Ndani Ya Miezi Minne


Na Lydia Churi-Mahakama, Dodoma
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewataka Majaji wa Mahakama Kuu kuwa tayari kusikiliza mashauriyatakayofunguliwa kutokana na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mweziOktoba mwaka huu.

Akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa baadhi ya waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu yaTanzania, Jaji Kiongozi amesema Mahakama itampangia Jaji yeyote kusikilizamashauri ya uchaguzi hivyo kila Jaji anapaswa kuwa na hali ya utayari nakujiandaa kutekeleza wajibu huo muhimu.

“Mafunzo mliyopata yana lengo la kuweka mazingira sahihi ili Jaji yeyote atakapopangiwa kusikiliza mashauri yatokanayo na uchaguzi Mkuu awe tayariwakati wote”, alisisitiza Jaji Kiongozi.

Alisema Mahakama imepanga kumaliza mashauri yatakayotokana na uchaguziMkuu wa mwaka huu ndani ya miezi minne (4) kwa kuwa tayari imeshaoneshamwelekeo wa kuyashughulikia. Aliongeza kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka2015 mashauri ya aiona hiyo yalisikilizwa na kumalizika ndani ya miezi sita (6)tangu kufunguliwa kwake.

Jaji Feleshi amewataka Majaji Wafawidhi kujiandaa na pia kuhakikisha wanawaandaa Naibu Wasajili pamoja na Mahakimu ili wawe tayari kusikilizamashauri hayo. Kiongozi huyo pia ameagiza mashauri mengine yaliyopo nayanayoendelea kufunguliwa mahakamani yaendelee kusikilizwa na kumalizikakwa wakati licha ya kuwepo kwa mashauri yatakayotokana na uchaguzi Mkuu.

Aidha, ametoa wito kwa Majaji wote kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao,kujaliana na kupendana wakati wote kwa kuwa mahakama ni familia.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana naChuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) yamesaidia kuwajengea uwezoMaafisa wa Mahakama na kuwaandaa kutoa haki kwenye mashauri ya UchaguziMkuu ujao wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Mafunzo yaliyomalizika jana yaliwahusisha baadhi ya Waheshimiwa Majaji waMahakama Kuu ya Tanzania. Awamu inayofuata pia itawahusisha Majaji wengine wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Jumatatu Agosti 24 yataanza mafunzo hayokwa Wasajili, Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama zaHakimu Mkazi.

Mafunzo haya pia yatatolewa kwa waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufanikuanzia Septemba 2-4, 2020 mkoani Morogoro. Mahakimu Wakazi Wafawidhi waMahakama za Wilaya nao watapatiwa mafunzo hayo baadaye katika Chuo chaUongozi wa Mahakama Lushoto-Tanga.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani naMahakama Kuu waliopo na wastaafu, Naibu wasajili, Mahakimu pamoja na wawezeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Kurekebisha Sheria ambao ni wadau muhumu katika masuala ya Uchaguzi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad