Kibarua cha TEMESA kimeota mbawa Simiyu.
0
August 12, 2020
Na Samirah Yusuph, Simiyu
Wakala wa ufundi na umeme nchini (TEMESA) imesitishwa kufanya kazi zake za ufundi kwa magari ya serikali mkoani simiyu kutokana na gharama zake za matengenezo kuwa juu.
Marufuku hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kumpa miezi mitatu afisa usafirishaji wa mkoa kuhakikisha kuwa ndani ya muda huo anafanya maandalizi ya kutosha.
"Hatuwezi kuvumilia ukipeleka gari TEMESA unalipa mara tatu zaidi ya bei za kawaida kwanini tuendelee kuwa nao hali kuwa kuna sehemu unaweza ukatumia pesa hiyo kutengeneza zaidi ya gari moja," alisema mtaka.
TEMESA ni wakala wa ufundi na umeme mwenye jukumu la kufanya matengenezo ya magari, piki piki na mitambo ya serikali katika karakana ambazo zipo kila mkoa.
Tags